Tuesday 19 July 2016

Profesa Mavura afariki dunia ndani ya ndege

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Arusha (JKUAT), Profesa Ward Mavura wakati wa uhai wake 
Dar es Salaam.  Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Arusha (JKUAT), Profesa Ward Mavura amefariki dunia leo wakati akiwa kwenye ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha.

Chanzo kimoja kilicho karibu na familia hiyo kimesema kuwa  Profesa Mavura alikuwa anatarajia kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Mwili wa Profesa Mavura umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana wakati shughuli za mipango ya kusafirisha mwili kwenda Usangi kwa dada yake zikifanyika.

No comments:

Post a Comment