Wednesday 13 July 2016

Celtic yaumbuliwa na timu ya waajiriwa wa Umma

Baadhi ya waajiriwa wa umma kutoka, Idara ya zimamoto, Forodha, na biashara ya usafirishaji abiria (Teksi), wa timu ya Gibraltar imeweza kuwaumbua vigogo wa Scottland, Celtic katika mechi za kufuzu michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Meneja mpya wa Celtic, Brendan Rodgers, amesema hakuna aibu katika timu yake kuchapwa kwa bao 1-0 na Lincoln Red Imps ya Gibraltar kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya mechi za mchujo kwa mashindano ya UEFA Champions League.

Goli lililofungwa na afisa wa jeshi la polisi Lee Casciaro lilisababisha Celtic kupoteza mechi hiyo, ambayo ilkuwa mechi ya kwanza ya ushindani ya kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers.

Baadhi ya wachezaji wa Lincoln Red Imps walikuwa Askari wa kuzima moto, dereva wa teksi, na afisa wa forodha, kitu ambacho kimeonekana ni fedheha kwa Waskotish hao kufungwa na timu ya namna hiyo.

Akizungumza kabla ya mchezo huo, Nahodha wa Lincoln, Chipolina, ambaye ni afisa forodha amesema ilikuwa ngumu kufanya kazi na kucheza mpira kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment