Saturday 16 July 2016

50 Cent amhimiza Kanye West agombee Urais wa Marekani 2020

Alipotangaza mwaka jana kuwa mwaka 2020 atagombea urais wa Marekani, watu wengi waliamini kuwa Kanye West alikuwa akiota ndoto za mchana.
Hata hivyo wapo watu ambao wanaamini kuwa Yeezy pamoja na kutokaukiwa vituko, anafaa kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo kubwa duniani. Mmoja wa watu hao ni 50 Cent, hasimu wake wa zamani.

“Nadhani Kanye anatakiwa kugombea,” 50 alisema kwenye podcast ya Drink Champs.

“Sijali kama atapoteza. Nataka tu agombee, watu hawawaamini wanasiasa hivyo watamuangalia na kumuona ni kitu tofauti na hata kama akifanya makosa, anasema anatenda katika ukweli.”
Kwenye show hiyo pia 50 alizungumzia bifu ya Meek Mill na Drake.

No comments:

Post a Comment