SerikaliYapanga Kufanya MatumiziYenye Tija

Na Mwandishi wetu
Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija
kwa kuelekeza Bajeti kubwa kwenye Mambo Muhimu hasa sekta zenye za
kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
Akiwasilisha Mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha
2016/2017 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema
mwongozo wa mpango na bajeti Umezingatia mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za
uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla
ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika
kipindi hiki.
“
Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla
ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1
ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa Mapato yasisiyo
ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion
1.1.
“
katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya
shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia
13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la Asilimia 14
ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3
kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
Mhe
Philip Mpango amesema Mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na
Mipango, hivyo Basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za
serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za
Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na
kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na
bajeti iliyoidhinishwa.
\
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya Mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na Mashirika mengine.
\
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya Mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na Mashirika mengine.
Serikali
itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na
kuelekeza matumizi kwenye Maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania
wote.
No comments:
Post a Comment