Na Tabu Mullah
Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.
Katika
mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za
mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting.
Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons
ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.
Kapombe
alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake
dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye
mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara
nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.
Washindani
wa Kapombe kwenye kinyang’anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa
mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa
Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.
Kwa
kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni
moja) na wadhamini wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania Limited.
FULL MKANDA PAMBANO LA CHEKA NA MSERBIA LEADERS JANA, CHEKA ASHINDA KWA …’.POINTI’
Bondia
Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia
kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12
la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku
wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Katika
raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya
mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini,
jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na
kisha kuendelea na pambano.
Baada
ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana
kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake
akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa
na madhara kwa Cheka.
Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi
Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake….
No comments:
Post a Comment