Wednesday, 17 February 2016

Naibu Waziri wa Afya na jinsia na Maendeleo Dkt Hamis Kigwangalla ameutaka Uongozi wa Hospital Ya Rufaa Ya Morogoro Kurekebisha Mapungufu yaliyopo


NAB1
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alisamiliana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu mara baada ya kuwasili mkoani  humo  jana  jioni kwa ajili ya kutembelea  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Morogoro.
NAB2
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia mfumo wa makusanyao ya mapato kwa  kutumia mtandao, ambao unafanya kazi sehemu ya usajili tu(mapokezi) kutokana na hali hiyo liagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha unagunga mtandao huo kwenye maeneo yote ya malipo ili kuhakikisha mapato hayapotei.Aliyekaa katika kompyuta ni Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Asteria Mbele na  kulia ni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt Rita Lyiyamuya.
NAB3
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia  jana baadhi ya vifaa vya maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .
NAB4
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia na kuhoji  ni sababua zipi zinazosababisha  mashine ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ,figo na ini (BIOCHEMIST) ambayo haifanyi  kazi   mara baada ya kutembelea  Hospitali  ya  Rufaa ya  Morogoro .Kushoto  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu.
NAB6NAB8
NAB9
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwaagiza kuhakikisha taa za vyumba vya upasuaji zinafanya kazi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu  ambapo alitoa muda wa siku  60 wakati alipotembelea  Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .Pia  alitoa muda wa miezi sita wa kufanya marekebisho ya baadhi ya majengo.

Wa KITWANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA ULAYA, WANANIA YA KUWEKEZA NCHINI, MAHUSUSI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

kit1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimfafanulia jambo Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) na Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), wakati wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa TPSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kit2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimsikiliza Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa majukumu mbalimbali wanayoyafanya katika kampuni yake.  Kulia kwake ni Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl. Wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kit3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Bara la Ulaya, ambao ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia), Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)-(ESSB), Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Wawekezaji hao walikutana katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment