WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na
Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi
ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na
Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi
ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.
Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo Kanisa na Msikiti zimeezuliwa mapaa
katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo imesabisha kaya hizo kukosa mahali pa kuishi , huku
wengi wa waathirika wakipewa hifadhi kwenye nyumba za majirani
zao.
wengi wa waathirika wakipewa hifadhi kwenye nyumba za majirani
zao.
Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji
cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo
January 27 mwaka huku saa kumi jioni.
cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo
January 27 mwaka huku saa kumi jioni.
Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni Vitongoji vya Kwemchaa,
Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio
vimeweza kuathirika na maafa hayo.
Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio
vimeweza kuathirika na maafa hayo.
Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa
wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa
kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa
kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo
anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada
zaidi.
anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada
zaidi.
“Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji
Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu mwingine” alisema Makamba
Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu mwingine” alisema Makamba
Makamba aliwataka wananchi wote kupanda miti ili kuepuka upepo
mkali unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika
maeneo tofauti
mkali unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika
maeneo tofauti
Suala LaAda Elekezi Kuhusisha Wadau Wote – Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye
kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na
likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana
(Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini
walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo
iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye
alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa
akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama
Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake
ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.
Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya
reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua Miundombinu hiyo na
kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo
husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la
kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora –
Kaliua – Mpanda hadi Karema.
“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa
Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya
tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini
Burundi Ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar
es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda
Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.
Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani
ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya
mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya
juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.
“Bunge ni eneo linaloweza kujenga
jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia
sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi
tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.
Kuhusu ombi la kuibuliwa upya
mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na
anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa
kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu
Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii
inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia
ubabe na mabavu au nguvu ya dola.
“Nimewaona baadhi ya wabunge mko
hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu.
Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe
Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una
kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,”
alisisitiza.
Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk.
Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa
upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya
watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.
“Mchakato huo ukianza utumike
kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia
Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria.
Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Askofu ambaye
amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema
anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa
hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.
“Si kwa akili na uwezo wangu bali
ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo.
Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na
kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya
matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na
roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.
Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais
Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo.
“Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea
kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,”
alisema.
No comments:
Post a Comment