Sehemu ya Barabara ya Morocco
kwenda Mwenge ikiwa katika hatua ya kutolewa tabaka ya Udongo wa
chini na kuwekwa tabaka ya udongo mpya kama inavyooenekana katika picha
leo jijini Dar es Salaam .
Mafundi kutoka kampuni ya
Ujenzi ya ESTIM wakiwa kazini katika hatua ya kutoa udongo wa chini
kwa ajili ya kuweka udongo mpya ,ambapo ujnzi huo unatarajiwa kumalika
mapema Mei mwaka huu.
Kipande cha Barabara ya
Mwenge-Morocco kilicho kamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la
Mwenge-Bamaga kinavyoonekana katika picha . (Picha na Lorietha Laurence
–Maelezo).
Mafundi wakijengea bomba la maji
eneo la Makumbusho kwa kuliwekea zege na nondo ili kulihakikishia
usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco
inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
Mafundi wakijengea bomba la maji
eneo la Makumbusho kwa kuliwekea zege na nondo ili kulihakikishia
usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco
inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala
wa Barabara Tanzania (TANROADS) Bi.Aisha Malima akipata maelezo kutoka
kwa Fundi Mchundo (Civil Technician) wa Kampuni ya Ujenzi ya ESTIM ,Bw.
Kano Warema kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco
leo jijini Dar es Salaam.
IGP Akiwaapisha Makamishna Wa Polisi Waliopandishwa Vyeo Na Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Simon Sirro baada
ya kupandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na kuwa
Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Albert Nyamuhanga
baada ya kupandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na
kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Fedha na
Logostiki wa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Robert Boaz baada
ya kupandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri wa Muungano ya
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na kuwa
Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Intelijensia wa
Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Nsato Marijani
baada ya kupandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa
Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
IGP Ernest Mangu (kushoto) akimpongeza Kamishna wa Operesheni na
Mafunzo, CP Nsato Marijani baada ya kumuapisha jana Makao makuu ya
Jeshi la Polisi. CP Nsato Marijani amepandishwa cheo na Mheshimiwa Rais
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia
amemteua kuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment