Afisa
Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha
akiwaeleza waandishi Wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ardhi oevu Duniani inayotarajiwa kufanyika
februari 2,2016 ambapo siku hiyo itatumika kutoa elimu kwa kuwakumbusha Watu kuhusu uhifadhi na Matumizi endelevu ya Rasilimali za ardhi oevu.
Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Lusungu Helela, kushoto ni
Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu Kitaifa wa Uhifadhi Ardhi Oevu Bw.
Pellage Kauzeni.
Afisa
Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw. Pellage
Kauzeni akitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya ardhi
oevu kushirikiana na Serikali katika kuyatunza maeneo hayo kushoto ni
Afisa Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha
na kulia ni Afisa Habari wa wizara hiyo Bw. Lusungu Helela.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatlia mkutano wa Wizara ya Mali Asili na
Utalii uliolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maadhimisho ya siku ya
ardhioevu ambayo huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe unaoweza
kusababishwa na mawimbi ya bahari.
Na Mwandishi wetu
MKUU
wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid amewataka walimu wakuu katika
wilaya hiyo , kusimamia upatikanaji wa hati miliki ya maeneo ya skuli
zao .
Amesema
kuwa Maeneo mengi ya Skuli ndani ya Wilaya ya Wete yanakabiliwa na
migogoro ya Ardhi inayosababishwa na kutokuwepo na hati miliki .
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na walimu Wakuu wa Wilaya hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Zamani wa Chuo cha uwalimu Benjamini Mkapa kwenye
mkutano wa kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo .
‘Kila
mwalimu analojukumu la kusimamia upimaji wa maeneo ya Skuli na kisha
kupatiwa hati miliki , hii itaondoa migogoro inayojitokeza kwa sasa
”alisisitiza
Amesema
kwamba Serikali ya Wilaya iko tayari kushirikiana na Uongozi wa Skuli
katika Wilaya hiyo kuhakikisha maeneo hayo yanapimwa na kupatiwa hati
miliki .
“Serikali
ya Wilaya iko tayari wakati wowote kutoa msaada wa uoatikanaji wa hati
miliki ya Maeneo ya Skuli , tunashirikiana kufuatilia katika ngazi
zinazohusika ”aliafahamisha.
Mapema
Afisa Elimu na Mafunz ya Amali Wilaya hiyo Khamis Said Hamad amesema
kwamba yapo Baadhi ya maeneo ya Skuli yamepimwa lakini imekuwa ni vigumu
kupatikana kwa hati miliki .
Hivyo Ameiomba Serikali ya Wilaya kusaidia kupatiokana hati miliki katika
Skuli hizo ambazo tayari maeneo yake yamepimwa ikiwa skuli ya Sekondari
ya Pandani .
“Zipo
skuli tayari maeneo yake yamepimwa lakini bado hati miliki
hazijapatikana , ikiwemo Skuli ya Sekondari ya Pandani ambayo eneo lake
limeshapimwa ”alifahamisha.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mchangamdogo Juma Said Hamad
ameiomba Serikali ya Wilaya kulipa kipaumbele suala la kuyapima maeneo
ya skuli .
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba asilimi 60 ya maeneo ya Skuli
za Wilaya ya Wete hayana hati miliki jambo ambalo linasababisha maeneo
hayo kuvamiwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na makaazi
No comments:
Post a Comment