Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa
ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini
hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan
Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa
Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze
kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja
wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa ma Mwanaidi Mussa na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya
Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia
shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma
za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Nape mgeni rasmi Tamasha la Pasaka Mwanza
WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha
la Pasaka jijini Mwanza Machi 27.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Waziri Nape amekubali
kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na
kumalizia Kahama Machi 28.
Msama alisema kamati yake
inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha
waimbaji mbalimbali hapa nchini.
“Maandalizi kuelekea Tamasha la
Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa
wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na
waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.
Msama alisema baadhi ya waimbaji
waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando,
Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila,
Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro
na Kwaya ya Wakorintho Wapili.
Aidha Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na kwa watoto shilingi 2000.
No comments:
Post a Comment