Wednesday, 24 February 2016

Mbunge wa Ismani William Lukuvi ametoa Msaada wa Pesa kwa Waathirika wa Mafuriko Idodi

DSC_0580
Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa  kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha  kiasi cha Tsh milioni 2 za  kulipa fidia  ya ardhi kwa  wananchi  watakaohamishiwa makazi mapya  kutoka  kitongoji  cha Kitanewa Idodi ambao  nyumba   zao zilisombwa na mafuriko
Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa Ardhi ,nyumba na Maendeleo ya makazi (kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi fedha hizo, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.

 Na Mwandishi Wetu
MBUNGE  wa jimbo  la  Isimani  Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole
waathirika  wa mafuriko wa kata  ya Mapogolo tarafa ya  Idodi wilaya ya 
Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada  wa pesa  zaidi ya Tsh 
milioni 9  kwa ajili ya kusaidia mahitaji  mbali mbali ikiwa ni pamoja 
na  kurejesha  miundo mbinu  ya maji  safi  iliyoharibiwa na mafuriko.
Bw Lukuvi  ambae  pia ni  waziri  wa Ardhi  ,nyumba na maendeleo ya makazi
 alikabidhi msaada  huo  jana  baada ya  kutembelea  waathirika  hao 
waliopo kambi  ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara  ya
kutoka Iringa  kuelekea hifadhi ya  Taifa ya Ruaha ambayo kwa   sasa
imekarabatiwa baada ya  awali barabara   hiyo kukatika kutokana na
mafuriko hayo , alisema   kuwa  lengo lake  kama mbunge  wa  jimbo  
hilo la Isimani na  serikali ni kuona  wananchi  waliokumbwa na
mafuriko   wanaendelea  kusaidiwa .

Alisema  kuwa  awali aliomba msaada  wa mahindi   tani 100  kutoka   serikali kwa
ajili ya waathirika  hao  wa mafuriko Idodi na  Pawaga  ikiwa ni  
pamoja na  kuwasaidia  msaada  wa  fedha   kiasi cha  zaidi ya Tsh
milioni 3 kwa ajili ya  kuwawezesha  waathirika  hao  wa mafuriko  
kupata mahitaji mengine kama mboga na  pesa ya  kusagia mahindi hayo .
Bw  Lukuvi alisema  kuwa kwa ajili ya kurejesha  huduma ya maji kijijini
hapo  amewasaidia kiasi cha Tsh  miliobni 4 ambazo  wameomba  kwa ajili
ya  kuboresha miundo mbinu  hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa  ajili
ya kukiwezesha   kijiji kulipa fidia ya ardhi  kwa  wananchi waliotoa
ardhi  yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha  Kitanewa ambao
wanapaswa  kuhamishwa eneo  hilo la mafuriko la  kupewa makazi mapya .

” Waambieni   watu  wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya
viwanja mwaka   huu  wavune mazao yao na  baada ya  hapo kila  mmoja 
muweze  kumlipa  fidia ya  Tsh 200,000 na  baada ya  hapo waitini 
Wataalamu  wa ardhi  ili  waweze  kupima  viwanja na  mpanfgilio  mzuri 
zaidi kwa  ajili ya makazi mapya …….pia nataka hata mashamba ya 
kawaida  ya wananchi kupimwa  ili kupata hati za ardhi
zitakazowawezesha  kutumia kupata mikopo ….ila  nitawaletea mashine
za  kufyatulia tofari ambazo  unaweza  kuzijengea  bila  kuchoma “
Alisema kuwa  kwa  ajili ya  kuhamasisha ujenzi  wa  nyumba   bora mwananchi
Atakayekuwa  wa kwanza  kupandisha  jengo atamchangia bati japo kwa 
sasa amekwisha  toa bati  zaidi ya 300 kwa  mkuu  wa wilaya ya  Iringa
kwa ajili ya  waathirika   hao.

Bw  Lukuvi  pia  amewapongeza wadau  mbali mbali zikiwemo taasisi za dini ,watu  binafsi
,Taasisi ya  kifedha pamoja na mifuko  ya  hifadhi  za  jamii  kwa 
kujitolea  misaada  mbali mbali kwa ajili ya waathirika  wa mafuriko na 
wagonjwa  wa Kipindupindu  Pawaga  .

Pamoja na  kuwashukuru wadau hao  Lukuvi  alimpongeza   waziri  Mkuu Kassim Majaliwa kwa    kuwatembelea waathirika  hao wa Mafuriko na  wale  wa Kipindupindu Pawaga .

Hata  hivyo  Lukuvi  alimpongeza  mkuu  wa wilaya ya  Iringa Bw Richard
Kasesela na  viongozi wote  akiwemo mkuu  wa mkoa Amina Masenza kwa  
kusimamia shughuli  mbali mbali  ikiwemo ya urejeshaji wa miundo mbinu
ya barabara   iliyokuwa  imekatika katika barabara ya Iringa – Ruaha .

Katika  hatua  nyingine  Bw  Lukuvi aliagiza  serikali ya  kijiji cha Mapogolo
kutowabagua  wananchi  katika  kugawa chakula   hicho  cha msaada na 
kutaka  hata  ambao  si waathirika  wa mafuriko ambao  wana njaa wapewe 
chakula   hicho  cha msaada kwa  waathirika wa mafuriko .
 
Wakati huo  huo Waziri Lukuvi  alisema  kuwa serikali inakusudia  kuijenga 
Barabara ya Iringa- kuelekea   hifadhi ya  Ruaha  kwa  kiwango cha  lami
kama  mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati  wa kampeni
kupitia ilani ya  uchaguzi ya CCM

Pia  kwa ajili ya  kuwafanya  wananchi  kunufaika watalii wanaotembelea
hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa alisema  tayari  jitihada za  kujenga
Viwanja  vidogo  vya ndege  nje ya  hifadhi ya  Ruaha  zimeanza na 
kuwa  lengo la  serikali ni  kuwahamisha wafanyakazi  wanaoishi  ndani
ya  hifadhi  hiyo na  kujumuika na  wananchi  nje ya  hifadhi ili 
waweze  kupata mahitaji kama  wananchi  wengine.

No comments:

Post a Comment