Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa habari kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Tarishi
Maimuna Kibenga. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Na Kalonga Kasati
Waziriwa Elimu,Sayansi,Teknolojia
na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa ajira wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega pamoja
nakuwasimamisha kazi Wakurugenzi watatu.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es
salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu
matatizo ya kiutendaji na matumizi mabaya ya
fedhazaUmmayanayofanyikaBodiyaMikopo.
Prof.Joyce Ndalichako amesema
kuwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo imeonesha utendaji usioridhisha kiasi
kwamba kumekuwa na matatizo mengina yanayojirudiarudia kwa wateja wao
mara kwa mara.
“Mikopo kwa wanafunzi imekuwa
ikichelewa kuwafikia bila sababu za msingi kiasi kwamba imejengeka
taswira kwa wanafunzi kwamba hadi walalamike wizara ni ndipo matatizo
yao yashughulikiwe hivyo, tatizo sio ukosefu wa fedha bali ni uzembe wa
watendaji katika kuwapatia wanafunzi mikopo yao kwa
wakati.”AlisemaNdalichako.
Amewataja watumishi
aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusuph
Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaj iMikopo Juma Chagonja pamoja na
Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo Onesmo Laizer.
Aidha,amezitaja baadhi ya sababu
zilizosababishwa kufukuzwa na kusimamishwa kazi kwa watumishi hao
zikiwemo za kufanya malipo yasiyo sahihi kwa baadhi ya wanafunzi
wanaosoma ndani na nje ya nchi pamoja udhaifu uliobaini kakatika mifuko
ya fedha.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
inajukumu la kutoa mikopo kwaajili ya wanafunzi wa elimu ya juu na
kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo, kwa mwaka wa masomo 2015/2016 jumla
ya Shillingi Bilioni 459 imetolewa mikopo kwa wanafunzi 122,486
wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kiingilio Cha Simba, Yanga Elfu Saba
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC
utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha
chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
Kiingilio cha juu cha mchezo huo
kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini
(20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya
machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza
kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF
(Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi
Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho
Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na
waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa
(Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha),
mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa
Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea
Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba (Taifa), Mbeya City v
Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu (Kambarage), Toto Africans v
Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting v Tanzania Prisons
(Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar (Majimaji).
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa
michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex,
huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa Nagwanda
Sijaon mjini Mtwara.
No comments:
Post a Comment