Monday, 22 February 2016

Trilioni 1 Za kusanywa kwa Mwezi februari Dkt Likwelile

MPO1
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee Mpoki Ulusubisya.
MPO2
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.
MPO3
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Ufundi Tarishi Kibenga amesema Wizara yake itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.
MPO4
Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
MPO5
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850.


Na Kalonga Kasati

Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa Zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu.

Amesema kuwa kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7  kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na ruzuku.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es salaam  imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo.
Aidha, Dkt. Likwelile amesema kuwa ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao  ,Wizara imetoa Shilingi Bilioni 1.65  kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. 

Kati ya fedha hizo  wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni Wametengewa  shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.

Ameongeza kuwa fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa Ajili Ya  Mishahara ya watumishi wa Umma  , Ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13. 

Fedha kwa ajili ya shughlui Mbalimbali za maendeleo zimetolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 166.2  Ambapo chuo kipya cha Sayansi kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mlunganzi la kimepatiwa Shilingi Bilioni 18 na Kiasi cha Shilingi Bilioni 13.6 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.
Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi Bilioni 23.078, Mpango wa Maji vijijini Bilioni l7.1, Maendeleo ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini Zimetengwa shilingi  bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama zimepatiwa shilingi bilioni 12.3. 

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa Makusanyo yameongeza kutoka shilingi trilioni 1.2  kwa mwezi Disemba hadi kufikia Trilioni 1.79 kwa mwezi Januari

No comments:

Post a Comment