Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi (Aliyekaa) akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa kikao chake na vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Na Kalonga Kasati
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (WatuwenyeUlemavu) Dkt Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuzingatia Sheria ya Watu wenye ulemavu kwa kuhabarisha kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kutoa habari,
Akitoa agizo hilo mbele ya vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuwakumbuka na watu wenye ulemavu katika utoaji wa taarifa mbalimbali katika Magazeti, Radio naTelevisheni hasa kwa kuzingatia lugha za alama ambazo zitawawezesha kuelewa habari husika.
“ Naomba tubadilike wanahabari kwa kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwahabarisha na wao pia, nawataka Wamiliki wa vyombo vya habari hususan Televisheni kuweka lugha za alama kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata habari mbalimbali zinazojiri katika taifa”
“Vyombo vya habari vinatakiwa kubadili uono wao juu ya walemavu na sio kwa kuangalia mambo hasi tu yahusiyo Walemavu kwamba wana shinda,hawawezi, wanahitaji msaada ila pia kwakuangalia mafanikio yao katika kuleta maendeleo ya taifa kiujumla” Alisema Dkt Possi.
Aidha Dkt Abdallah Possi amewataka waandishi wa habari hasa wa magazeti kuzingatia lugha wanazotumia kandika habari za watu wenye ulemavu ili kuondoa fikra na dhana hasi na unyayapaa juu ya walemavu huku Akitolea mfano baadhi ya lugha zinazotumika na baadhi ya waandishi katika kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu kuwa hazistahili.
Ametaja mfano wa lugha ambazo sio sahihi katika uandishi wa habari za wenye ulemavu mfano maneno vipofu, viziwi,vilema na maneno mengine bali wanatakiwa kutumia maneno yenye staa na yasiyoleta picha ya unyanyapaa Na udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa na udhalilishaji wa watu wenye ulemavu.
Kupata habari ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria No 9 ya Mwaka 2010 inavitaka vyombo vya habari kuhabarisha watu bila kuwabagua watu wenye ulemavu, tuelewe kwamba pia watu wenye ulemavu wana haki ya kupata taarifa kama watu wengine.
No comments:
Post a Comment