Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura ((wa nne
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa
TFF, BMT na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya
kumaliza wa kikao kilichofanyika ofisinii kwake leo jijini Dar es
Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya
mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya
Tiketi wakati wa mechi kwenye uwanja wa Taifa.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza
katika kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo
jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadili suala la matumizi ya mashine
za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi
wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi na kulia ni Meneja wa Uwanja wa
Taifa Rish Urio.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifuatilia
maelezo kutoka kwa Muhasibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Rose Janeth
Bandisa (kulia) wakati wa kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya
kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya
mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa
Taifa.Katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
Katibu Mkuu wa TFF Celestine
Mwesiga (kushoto) na Muhasibu Mwandamizi wa TFF Bw. Daniel Msangi
wakifuatilia kwa makini wakati wa kikao baina yao na Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura
(hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) akizungumza katika kikao baina ya Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura
(katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam.Kulia
ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kikao baina ya
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia
James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
MAGUGU MAJI YATISHIA HUDUMA ZA USAFIRI ENEO LA KAMANGA FERRY JIJINI MWANZA.
Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya.
Suala
la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha
ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya
Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa
Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.
Mara
kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji
ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.
Usumbufu
kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry
Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda
katika eneo hilo.
Kumbuka
Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana
na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini
ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.
Suala
kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea
ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa
Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale
vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.
Hata
hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho
maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo
ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi
ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za
kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
Wakaazi wa kisiwa cha Mtambwe Mkuu Wilaya ya Wete waomba taasisi za kupambana na uharibifu wa mazingira kuelekeza nguvu kisiwani humo
Na Tabu Mullah
WAKAAZI wa kisiwa cha Mtambwe Mkuu Wilaya ya Wete wameziomba taasisi zinazoh
usika na suala la utunzani wa mazingira kuelekeza nguvu katika kisiwa hicho ambacho kiko hatarini kutoweka .
usika na suala la utunzani wa mazingira kuelekeza nguvu katika kisiwa hicho ambacho kiko hatarini kutoweka .
Wamesema kwamba kisiwa hicho kimekuwa kikiliwa na maji ya bahari siku ha siku , na kusababisha eneo la kisiwa hicho kupungua kwa kasi .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema iwapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa na Serikali pamoja na taasisi husika , historia ya kisiwa hicho itapotea .
“Kisiwa hichi kinahistoria kubwa , lakini inaweza ikapotea kutokana na bahari kuendelea kuvamia ardhi ya kilimo na makaazi , tunaomba nguvu katika kufanikisha hili ”alisema Alawi .
Sheha wa Shehia ya Mtambwe Kaskazini Bakar Khamis Suleiman ameiomba Serikali pamoja na taasisi binafsi kuweka mkazo wa kupanda miti ya kudumu kwenye eneo la kisiwa hicho .
Sheha Bakar amesema wakaazi wa kisiwa hicho wamekuwa wakipanda miti , lakini kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha miti imeshindwa kutatua tatizo hilo .
“Kipo kikundi cha upandaji wa miti katika Kisiwa hichi , lakini mafanikio hayapafikiwa kutokana na wanakikundi hao kukosa taaluma na miti wanayopanda imeshindwa kutatua tatizo ”alifahamisha .
Inakisiwa kwamba eneo la zaidi ya mita ishirini na nchi kavu zimekuwa himaya ya bahari katika Kisiwa hicho , ambapo miti aina ya miembe na minazi nayo ikiwa imeng’olewa na mawimbi ya bahari .
Kwa upande Mwenyekiti wa Jumuiya ya wandishi wa Habari wa Mazingira Pemba Azizi Smail Alawi ameahidi kuwa Jumuiya yake imejipanga kutoa elimu ya upandaji wa miti hasa maeneo ya visiwa vidogo vidogo .
Amesema kwamba shehia nyingi ambazo ziko kando kando ya bahari , zimevamiliwa na maji na kuzitaja kuwa ni Msuka ,Mjini Kiuyu pamoja na Kisiwa Panza
No comments:
Post a Comment