Saturday, 20 February 2016

Tamasha la pasaka kiingilio ni 5000 Kwa Wakubwa Na 2000 Kwa Watoto

2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na Waandishiwa habari wakati alipotangaza viingilia vya tamasha la Pasaka litakalofanyika katika Mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga, kushoto ni  Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Khamis Pembe.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions imetangaza viingilio vya Tamasha la Pasaka mwaka huu kuwa ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama alisema viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.

“Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.

Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi Wa Mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa baiskeli zaidi ya 100 za walemavu ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.

Aidha Msama alisema Waimbaji mbalimbali wamethibitisha  kushiriki tamasha hilo ambao Wanaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa.

Naye Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Khamis Pembe alisema wanaendelea na Mikakati ya kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa mikoa hiyo.

Ofisi Ya Mbunge Wa Viti maalum (CHADEMA) Mkoani Mwanza Kuzinduliwa  Rasmi Hii Leo.

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa na Taifa hii leo wanatarajia kuzindua Rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Jimboni Ilemela.
 
Uzinduzi huo utaambana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. Pichani juu ni Secretary wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Pichani ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke.
Kushoto ni Ofisi ya Katibu  (Mwenye Miwani) wa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) na Kulia ni Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA).
Jengo la Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Rasmi hii leo. Ofisi hii iko GreenView, Mtaa wa Ghana Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza

No comments:

Post a Comment