Shirikisho la soka
duniani Fifa litampta kiongozi mpya leo wajumbe 207 watakapokusanyika
mjini Zurich, Uswizi kumchagua mrithi wa Sepp Blatter.
Aling’atuka mwaka Jana kutokana na Tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo.
Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi.
Watano hao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne.
Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda.
Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki).
Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe.
Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa.
Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na anayepata kura nyingi kutangazwa Mshindi.
Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi Raundi ya pili.
Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.
No comments:
Post a Comment