Na. Tabu Mullah
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki
amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said
Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake
Mhe. Kairuki ametoa maamuzi hayo
leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano na waandishi wa Habari katika
moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.
“Namsimamisha Bwana Said Nassoro
aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia Watumishi walioko
chini yake na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo
hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,”
alisema Mhe. Kairuki.
Mhe. Kairuki aliongeza kwa kusema
kuwa Usimamizi wa Bw. Nassoro ambao Haukuwa wa Ufanisi Umetoa Mwanya
kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya Ubadhilifu wa mali za Umma Ambapo Mwaka 2011 na 2013 Aliyekuwa Mkurugenzi wa chuo Upande wa Tawi
la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za Ujenzi.
Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU Zilithibitisha
ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote
badala Yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na
kuendelea na wadhifa wake.
Kutokana na ubadhilifu huo
imempelekea Mhe. Kairuki kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye Alikuwa
Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph
Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha
shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka
wa fedha 2014/15.
Mhe. Kairuki ameendelea kueleza
kuwa bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao Hawafuati
mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza watumishi ambao Wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na miongozo ya Utumishi wa
Umma kwa ukamilifu wake.
Waziri Muhongo aitaka TANESCO na TPDC kufanya kazi kisasa
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya
Pan African Energy Andy Hanna ( wa pili kutoka kulia) akielezea majukumu
ya kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na
Taasisi zilizopo chini yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya gesi nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya
Pan African Energy Andy Hanna (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Pan
African Energy Nchini Patrick Rutabanzibwa (kulia) wakinukuu maelekezo
kutoka kwa Wiziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo
pichani)
Na Tabu Mullah
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kufanya kazi katika
mtindo wa Kisasa ili nishati ya umeme iweze kuwa ya uhakika kwa
maendeleo ya uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo
katika kikao chake na Kampuni ya Pan African Energy kilichofanyika
jijini Dar es Salaam kilichoshirikisha pia watendaji kutoka wizara ya
nishati na Madini, TANESCO, TPDC na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA).
Alisema Mahitaji ya gesi kwa
ajili ya kuzalisha umeme wa uhakika ni makubwa, hivyo hakuna Sababu ya
kuwepo kwa upungufu wa nishati ya umeme nchini wakati kuna gesi ya
uhakika.
Alifafanua kuwa haiwezekani
shirika la TPDC likadai kuwa kuna gesi ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha
umeme, wakati kuna Upungufu wa umeme nchini.
Alisema serikali ina mpango wa
kuhakikisha kuwa Wananchi wote hasa waishio vijijini Wanaunganishwa na
umeme wa uhakika kupitia Wakala wa Nishati Nchini (REA) hivyo ni jukumu
la mashirika hayo kuhakikisha yanabuni miradi na kukaribisha wawekezaji
mbalimbali katika Uzalishaji wa umeme wa uhakika ili wananchi wote Waweze kuunganishwa na huduma ya umeme
.
Alisisitiza kuwa amekwishawaalika
wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza kwenye Uzalishaji wa
Megawati 1000 za umeme kwa ajili ya kuingizwa kwenye gridi ya taifa,
hivyo ni vyema shirika la TPDC likahakikisha gesi ya uhakika
inapatikana ili umeme uweze kuzalishwa mara moja.
“ Lengo la serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025
Megawati 10,000 zinazalishwa, hivyo sekta ya nishati kuchangia ukuaji
wa uchumi wa nchi Na kutoka kwenye kundi la nchi masikini duniani na
kuingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati, kama Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025, inavyofafanua,”alisema Profesa Muhongo.
Wakati huo huo, Profesa Muhongo
aliitaka kampuni ya Pan Afrian Energy kuhakikisha inatatua Changamoto
zote inazozikabili kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya kukutana
naye Juni 01 Mwaka huu kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya kampuni hiyo
katika kuzalisha gesi ya uhakika.
Alisisitiza kuwa kutakuwepo na
utaratibu wa kukutana na kampuni hiyo kila baada ya miezi mitatu kwa
ajili ya kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo, na serikali ipo tayari
kutoa msaada pale kampuni itakapokwama.
Aidha, Profesa Muhongo aliitaka
kampuni hiyo kuweka utaratibu wa kuajiri vijana wa kitanzania Wanaomaliza masomo ndani na nje ya nchi baada ya kupata ufadhili kutoka
serikalini.
“ Kwa sasa tuna vijana wengi
waliohitimu mafunzo kwa ngazi ya shahada za uzamili katika Masuala ya
mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kama Norway,
Uingereza Na China, hivyo ni vyema wakapata ajira katika kampuni ya
Pan African Energy, ili nao waweze kufaidika na elimu na uwepo wa
uwekezaji katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na Mafuta
nchini,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni
ya Pan African Energy Andy Hanna, akielezea mafanikio ya uwekezaji
kupitia kampuni yake, alieleza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutoa
ajira 87 kwa Watanzania na kuboresha huduma za jamii kama vile kutoa
huduma ya umeme bure katika eneo la Kilwa kilipo kituo chake za
kuzalisha gesi.
Aliendelea kusema kuwa kampuni ya
Pan African Energy imejenga zahanati pamoja na kutoa Mafunzo kwa
waajiriwa wake lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakuwa na
wataalam wazawa.
No comments:
Post a Comment