Friday, 19 February 2016

Kocha Kinnah Phiri wa Mbeya City Amesema Anajua Azam FC ni Timu nzuri, lakini kesho ‘Watamuwia Radhi Atawafunga



 Kocha Kinnah Phiri wa Mbeya City



 KOCHA Kinnah Phiri wa Mbeya City amesema anajua Azam FC ni timu nzuri, lakini kesho ‘watamuwia Radhi’ atawafunga tu katika harakati zake za kuinusuru Timu yake isishuke daraja.
 
Akizungumza na Fofam-media Blog  Phiri kocha wa Zamani wa Free State Stars ya Afrika Kusini amesema kwamba vijana wake wako vizuri kuelekea mchezo wa kesho Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.  
 
“Itakuwa mechi nzuri, vijana wangu baada ya matokeo mazuri wiki iliyopita tukiwafunga 5-0 Toto Africans, sasa wamehamasika zaidi. Natarajia matokeo mazuri,”amesema Phiri.
 
Akiizungumzia Azam FC, Phiri amesema anajua ina wachezaji wazuri wengi, lakini yeye anamjua vizuri Nahodha wao tu, John Bocco. “Mimi nitacheza kwa kujiamini Mfumo wa kushambulia, ninataka ushindi, lazima nishambulie,”amesema Phiri.
Phiri alianza vizuri kazi Mbeya City baada ya kuifunga Toto African ya Mwanza Mabao 5-0 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi iliyopita na kesho atakuwa Na mtihani mwingine mbele ya kocha Muingereza, Stewart Hall. 
 
Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa Michezo sita kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini, ingawa macho na masikio ya wengi vitaelekezwa Uwanja wa Taifa, Dar e Salaam, ambako watani wa jadi, Simba na Yanga watakuwa wanamenyana.
 
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mgambo JKT wataikaribisha Tanzania Prisons, Uwanja wa Kamabarage Shinyanga Stand United wataikaribisha JKT Ruvu, Uwanja wa Majimaji Songea, Majimaji wataikaribisha Mtibwa Sugar na Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Toto Africans watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar.
 
Keshokutwa kutakuwa na michezo miwili ya kukamilisha mzunguko wa 20 wa ligi Hiyo, kati ya Ndanda FC na African Sport Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Mwadui FC dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.












No comments:

Post a Comment