Wednesday, 17 February 2016

Aliyetembea kwa miguu kutoka Mwanza Kumpongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli

ir1
 Katibu wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali akiwa ofisini kwake
siku kadhaa zimepita toka kufanyike uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la manispaa ya iringa kwa ajiri ya kujadili baadhi ya agenda za kulijenga upya baraza hilo,lakini chama cha walimu manispaa ya iringa kimegoma kuhudhuria baraza hilo kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali.
Akizungumza na blog hii katibu wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali amesema kuwa sababu ya kugoma kuingia kwenye baraza  la halmashauri ya manispaa ya iringa kwa kuwa baraza hilo limepitwa na muda hivyo kunaitajika kuliunda baraza jipya ndio waweze kuingia kwenye baraza la wafanyakazi.
Aidha katibu Njalali amesema kuwa wamekuwa wakiingia kwenye baraza la wafanyakazi kinyume cha sheria kwa majadiliano maalumu hivyo walikuwa wakihudhuria baraza batili na walikuwa wakimuambia mkurungezi juu ya swala hilo.
Njalali amesema kuwa haiwezekani baraza la wafanyakazi likawa na viongozi wengi kuliko wafanyakazi wenyewe hivyo watakuwa hawawatendei haki kwa kuwa hawatakuwa na hoja za msingi zinazowahusu wafanyakazi wenyewe.
“Angalia humu kwenye baraza hili tumejaa viongozi tu watumishe au walimu wenyewe wanawakilishwa na nani na tutengemee matokeo gani kwa miaka ya baadae kwa kupitisha bajeti isiyokuwa na mashiko kwa wahusika”.alisema Njalali
Njalali ameongeza kuwa hawawezi kuingia kwenye baraza la wafanyakazi ambalo halina viongozi kwa kuwa viongozi waliopo hawana uwezo wa kuwa viongozi wa kuongoza baraza hilo kutokana na uwezo wao wa kitendaji.
“Hatuwezi kuongozwa na wajumbe na viongozi haramu kwa kuwa wamekiuka sheria  na wanaijua hilo na kama mkurugenzi atandesha baraza hilo basi baraza hilo litakuwa batili kwa kuwa chama cha walimu ndio waliosaini mkataba huo”.alisema Njalali
Lakini Njalalia ametangaza rasmi mgogoro na mkurungezi wa manispaa ya iringa kwa kukiuka makubaliona waliokubaliana hapo awali wakati wa kusaini mkataba na kuwahidi walimu kuwa watampeleka mkurugezi CMA
“Nimemwandikia barua kuwa nimetangaza mgogoro na mkurugezi na nimempa siku tano kukutana na viongozi wa chama cha walimu manispaa ya iringa vinginevyo tarehe kumi na sita mwezi huu nampeleka kwenye baraza la usuruhishi CMA kwa kukiuka sheria na makubailiona ya mkataba wetu”.alisema Njalali
Njalali alimalizia kwa kusema kuwa baraza la wafanyakazi linafaida kwa watumishi kwa kuwa wanajadiliana na muaji wao juu ya mazingira ya kazi yao na wafanya nini ili kuboresha ufanyaji wa kazi zao na kuongeza ubunifu wa kuboresha kazi.
“Tumekuwa tunapitisha bajeti nyingi lakini hakuna mrejesho wowote ule wa ile bajeti tunayoipitisha  hivyo tumekuwa tunaburuzwa mara kwa mara kwa sasa basi hatutaki kuburuzwa tena tunataka haki yetu na ndio maana tumetangaza mgogoro na mkurugenzi wa manispaa ya iringa”alisema Njalali.
Tulipomtafuta mkurugezi wa manispaa ya iringa hakupatika kujibia kero hii iliyotolewa na katibu wa CWT,hata hivyo baraza la wafanyakazi lilifanyika na wakafanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.

BaSATA LAMPONGEZA MSANII 

tem1Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) (Kushoto) akizungumza na Msanii Joseph Stanford ofisini kwake mapema wiki hii. Msanii huyu ametembea kwa miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limempongeza Msanii Joseph Stanford kutoka Mwanza aliyetembea kwa miguu Umbali wa zaidi ya kilometa 1200 kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake pia uundaji wa Idara ya Sanaa iliyo chini ya Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni.
Aidha, BASATA imempa zawadi ya usajili bure msanii huyu ili atambuliwe rasmi katika tasnia ya Sanaa na baadaye kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta hii.
Akizungumza ofisini kwake, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kuwa Stanford ameonesha Uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake kwani haikuwa kazi rahisi kutembea umbali mrefu na usiku na mchana kuja kumpongeza Rais Dkt. Magufuli.
“Sisi kama Baraza tunafarijika sana, tunafurahi kuona wasanii na vijana kwa ujumla mnakuwa wazalendo na kufurahishwa na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano. Tunafurahi zaidi unapopeleka ujumbe wa Wasanii kwamba wamefurahia  kuundwa kwa idara ya Sanaa” alisema.
Aliongeza kuwa BASATA limetambua uzalendo na moyo wake wa kuipenda Sanaa hivyo limeamua kumpa zawadi ya usajili bure ili iwe chachu ya kujikita kwenye Sanaa na kufanya kazi zake kwa weledi na kuzingatia maadili ya kitanzania.
Kwa upande wake kijana Stanford alisema kwamba anafurahia kwa mapokezi aliyopewa na BASATA huku Akisisitiza kuwa ndoto yake ni kumfikishia salamu za pongezi Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli lakini pia kupata mafanikio kwenye kazi za Sanaa.
“Nafurahi sana kwa mapokezi niliyopata, muda wowote nitaenda kumfikishia salamu za pongezi Rais wangu. Matumaini yangu ni kuona sekta ya Sanaa inazidi kuthaminiwa na kusonga mbele” alisisitiza Stanford.
Msanii Stanford anatokea eneo la Mabatini jijini Mwanza na ametembea kwa siku ishirini na tano kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam na ametumia kiasi cha shilingi elfu arobaini na tano pekee

No comments:

Post a Comment