Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi (aliyesimama) akitoa neno la
ukaribisho kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe
(MB) katika tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11
waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa
mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiongeawakati wa tukio la kuachia
huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi
sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akielekea
katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya tukio la kuachia huru kundi la
sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma
maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akikata utepe
kuruhusu kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa
miezi sita kutoka nje kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha
ya pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti
kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya
kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo
mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru kundi la sita la mbwa 17
waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili kurejea katika makazi yao
ya asili.
Profesa Maghembe amesema serikali
itaendelea kuwekeza katika eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya
uhifadhi nchini kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema
mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na
kuwa wanyama wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema
uwekezaji mkubwa ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna
ambavyo uhifadhi unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu
unalenga kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao
walitoweka kabisa tangu mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo
hazijaweza kubainika kisayansi. Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na
watafiti wa kitanzania.
Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka
2011, jumla ya makundi sita ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya
Hifadhi ya Serengeti. Makundi haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni
hii ya simu ilifadhili gharama za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete;
Nyasirori na hili la mwisho ambalo lilipewa jina la Markus Borner,
mwanasayansi kutoka nchini Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya
shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti.
Mradi wa mbwa mwitu Serengeti
unaendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.
Katibu Mkuu Mambo Ya Ndani Ya Nchi Atembelea Vituo Vya Uhamiaji Vya Mipakani Mkoa Wa Kilimanjaro
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji
mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe
akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la
Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo
mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya
mipakani mkoani humo.
Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa
Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kulia) akimkaribisha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kulia) wakati alipowasili katika Jengo la Kituo cha
Pamoja cha huduma mpakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea mipaka ya Uhamiaji mkoani
humo Watatu kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria
Lembeli.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu)
azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma
katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa
wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa
ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu)
akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa
huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani
Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake
aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea
maendeleo nchi yao.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji
mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia)
moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma
Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto
ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali
Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji
vya mipakani mkoani Kilimanjaro.
Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa
Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto) akimuonyesha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji la
nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la
Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa
Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa
kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani
Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara
yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa
serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa
Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na
Kulia ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani
Holili, Aden Mwakalobo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Mbarawa Asisitiza Ukusanyaji Wa Mapato Katika Sekta Ya Miundombinu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na mkandarasi Nyanza Road
Works anayejenga barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51. (Wa
kwanza kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bw. Joshua Mirumbe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kisolya kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye
urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa barabara ya
Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami
ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda hadi Nansio Km 121.9.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Emmanuel Koroso (wa pili
kulia) wakati akikagua daraja la Kyarano linalounganisha barabara ya
Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km 467.7.
Muonekano wa daraja la Kyarano
linalounganisha barabara ya Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km
467.7 likiwa katika hatua za ujenzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na watumishi wa sekta za
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) kuhusu kufanya kazi kwa
umoja na kuongeza mapato katika sekta zao, mkoani Mara.
Meneja wa uwanja wa ndege wa
Musoma Bi. Bertha Bankwa akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika mkutano wa watumishi wa
sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.
Daraja la reli linaloingia
baharini katika bandari ya Musoma kupokea na kupakia mizigo kwenye
melikwa ajili ya kuisafirisha katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya
nchi.
Na Yahya Njenge
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji walio chini ya
Wizara yake kuongeza kasi ya kukusanya mapato ili kuwezesha malengo ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya
wananchi kufikiwa kwa wakati.
Akizungumza na watumishi wa sekta
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino mjini Musoma, Prof. Makame Mbarawa
amesema kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, uwazi na ubunifu kutasababisha
kufikiwa kwa malengo hayo mapema.
“Kama mtu hawezi kufanya kazi kwa
kasi na kwa malengo yanayotekelezeka na kupimika Atupishe kabla
hatujamuondoa, hatuta muonea mtu na hatutamvumilia mtu atakayeshindwa
kuendana na kasi yetu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema Serikali
imetenga zaidi ya dola milioni 30 kwa ajili ya kukarabati Uwanja wa
ndege wa Musoma na kununua magari ya kisasa ya zimamoto ili kurudisha
hadhi ya uwanja huo.
Aidha, amezitaka taasisi za
Serikali zinazodaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Mara
kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo kufanya kazi kwa kasi na
kufikia malengo yaliyowekwa.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata-Mto wa Mbu yenye
urefu wa km 467.7 inayojengwa na makandarasi wazalendo kumi na kutaka Mkandarasi anayejenga kipande cha km50 kutoka Makutano hadi Sanzate
kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa haraka ikiwemo daraja la kyarano
ili kuiwezesha barabara hiyo kupitika wakati wote wa mwaka.
Amemwagiza Meneja Wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa Mara Eng. Emmanuel Koroso kuhakikisha
makandarasi wanaojenga barabara mkoani humo wanarejea kazini kwa kuwa
serikali imeanza kulipa madai yao.
Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya
Butiama kutumia fedha zilizotumwa kutoka Mfuko wa Barabara (RFB)
kutumika kwa miradi iliyokusudiwa ili kuingunisha wilaya hiyo mpya na
wilaya nyingine mkoani Mara kwa barabara za lami.
Akiwa wilayani Bunda Prof.
Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga Barabara ya
Buliamba-Kisolya Km 51 kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kwa mujibu
wa Mkataba kwani serikali imeshalipa fedha shilingi bilioni 8.5 kwa
ajili ya barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara ya
Nyamuswa-Bunda-Kisolya-Nansio yenye urefu wa Km 121.9.
Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya za Magu,
Bunda na Musoma kufanya kampeni kubwa ya kuwaelimisha wananchi umuhimu
wa kulinda Miundombinu ya Barabara, Reli na Mkongo wa taifa wa
Mawasiliano ili isihujumiwe na kusababisha usumbufu kwa jamii na
kuisababishia serikali hasara.
Naye, Mbunge wa Mwibara Mhe.
Kangi Lugola amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kukamilika kwa
barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya hadi Nansio yenye urefu wa KM 121.9
itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Bunda na Ukerewe kwa kuwa eneo hilo
lina shughuli nyingi za uchumi zinazotokana na kilimo, ufugaji na uvuvi
wa Samaki.
Prof. Mbarawa amewataka
makandarasi wote nchini kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao mikataba
kulingana na sheria za nchi ili kuwezesha miradi ya barabara
inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati na kuondokana na hujuma
zinazoweza kudhoofisha ujenzi wa barabara na miundombinu mingine.
“Lindeni miundombinu ili idumu
kwa muda mrefu, barabara, reli na mkongo wa taifa ni Miongoni mwa
miundombinu inayojengwa kwa fedha nyingi na kuhujumiwa mara kwa mara
hivyo kuisababishia Serikali hasara”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye
ziara ya kukagua Ujenzi wa miundombinu ya barabara, Bandari na mkongo wa
taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo Ametembelea
Wilaya za Magu, Bunda, Butiama na Musoma.
No comments:
Post a Comment