Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Kikwete ameungana na wakazi wa vijiji vitatu vya
Kidogozelo,Kitonga na Milo,kata ya Vigwaza ,kukataa kukabidhiwa mradi wa
maji uliogharimu kiasi cha sh.Mil 258 fedha kutoka bank ya dunia .
Mradi huo umekataliwa kutokana na
kutokamilika pamoja na kuonekana mapungufu makubwa ikiwa ni pamoja na
mabomba kuwekwa karibu na ardhi,kupasuka kabla ya matumizi na kutandazwa
mabomba madogo yasiyokdhi mahitaji.
Kutokana na kasoro hizo kubainika
Ridhiwani ametoa mwezi mmoja kwa idara ya maji halmashuari ya wilaya ya
Bagamoyo kuhakikisha inafanya marekebisho na ukaguzi wa kina .
Hayo yalijiri juzi,baada ya
wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambao waliambatana na
wahandisi kutoka wizara ya maji kumuita mbunge huyo kwa malengo ya
makabidhiano ya mradi katika vijiji hivyo.
Akizungumza na wakazi wa vijiji
hivyo,Ridhiwani alisema yeye yupo pamoja nao na hawezi kukubali kukubali
kupokea mradi ambao una kasoro.
Alitoa siku 30 kupisha
marekebisho na ukaguzi na kusema endapo ataridhishwa na marekebisho
yatakayofanyika ndipo watakubali kuupokea.
Akielezea kuhusu mradi
huo,Ridhiwani alisema ulikuwa wa awali ambapo ulianza mwaka 1997 na
kugharimu Mil. 258 kwa fedha za ufadhili kutoka bank ya dunia ambapo
2013 ikiwa ni miaka miaka mitatu sasa ulipaswa ukabidhiwe baada ya
kufanyiwa maboresho .
Ridhiwani aliwataka
wakandarasi,watalaamu na mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya
wilaya ya Bagamoyo,Juliana Msagala kuacha masihala kwenye miradi
mikubwa inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha kutoka serikali na kwa
wahisani .
“Hili jambo sio jema
linasababisha wananchi wachukie serikali yao hivyo sisi wenye dhama ya
uongozi wajibu wetu ni kuona serikali inaendelea kukaa kwenye sura
nzuri na wananchi wakiendelea kujenga imani na serikali yao”
“Mradi huu umeanza 1997 tangu
mimi nikiwa namaliza kidato cha nne hadi leo jamani ,hebu rudisha miaka
nyuma ni miaka mingapi,wataala jaribuni kufanya kazi kwa maslahi ya
jamii na sio kwa maslahi mengine yasiyo na tija”alisema Ridhiwani.
Hata hivyo Ridhiwani alisema oct
2015 mradi huo ulitakiwa ukabidhiwe kwa mara ya kwanza lakini kwenye
ziara ya kamati ya siasa CCM walipita na kuona kasoro mbalimbali na
kamati hiyo ilikataa kukabidhiwa .
“Mabomba yalikuwa yanapasuka kwa
maana pampu ilikuwa kubwa jawabu ilikuwa kuweka mabomba yanayofanana na
pampu ile na sio kuweka mabomba madogo ya inchi mbili ama tatu ,ni moja
kati ya mapungufu,alielezea Ridhiwani.
Alitaja tatizo jingine maji
yakijaa wakati wa mvua yakipita kitonga na kufunga barabara ya milo
kutokana na mabomba kuchimbwa juu badala ya chini.
Awali Diwani wa kata ya Vigwaza
,Muhsin Baruhan alitoa kasoro mradi huo kutokana na kutotoa maji pamoja
na maeneo mengine kuonyesha mipasuko ya mabomba kabla ya kutumiwa na
vijiji lengwa.
Alisema wananchi wa vijiji
vilivyo ndani ya mradi wanapata tabu hivyo aliwaomba wataalamu kuwa
huruma na maisha ya watu ambao wanateseka.
Baruhan alielezea kuwa tayari alishapeleka taarifa za mapungufu ya mradi katika idara husika lakini utekelezaji ndio tatizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
kijiji cha Kidogozelo Ally Mmanga ,kutokana na mradi huo kusuasua
kunasababisha wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya madimbwi na mtoni
hivyo kuhofia milipuko ya magonjwa na kuliwa na mamba.
Mmanga alisema wanafunzi wa shule
hutumia makaratasi kujifutia mara baada ya kujisaidia jambo ambalo
linatishia usalama wa afya zao.
Mmoja wa wakazi ,Abdul Saidi
mkazi wa Kidogozelo ,alisema bomba lililofungwa ni la inchi mbili ambalo
haliwezi kusambaza maji katika mtandao wa vijiji sita hadi kumi kwani
kwa kufanya hivyo ni kusababisha maji kutoka kama mkojo.
Katika hatua nyingine mhandisi wa
idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msagala
anasema mradi huo umekamilika kulingana na mkataba licha ya kuhitajika
maboresho.
Alisema mradi huo uliingizwa
kwenye mpango wa uboreshaji wa mradi katika program ya maji usafi na
mazingira vijijini Kidogozelo iliingia katika program ya vijiji 10
ambapo halmashauri iliingia mkataba na mkandarasi Sajo Engineering
Contractor kwa ghamara ya sh mil.258.
Hata hivyo Juliana alisema
halmashauri hiyo itamkata mhandisi mshauri mil 18.345 kwa hasara
iliyosababishwa na usanifu usio sahihi.
Alisema fedha hizo zitatumika kurudisha mradi wa zamani na kuongeza mtandao wa mabomba katika vijiji vya Kitonga na Kidogozelo.
Mhandisi huyo alikiri kuwepo kwa
mapungufu yaliyoonekana na kumuahidi mbunge wa Chalinze Ridhiwani kuwa
maagizo aliyoyatoa watayafanyia kazi .
No comments:
Post a Comment