RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari
aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi waliojitokeza kwa wingi
kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.
Picha na IKULU
AFISA UHUSIANO TTCL AFARIKI DUNIA
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga
OFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga, amefariki dunia ghafla
usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016.
Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus
“…Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na
umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake..
Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua,” alisema Bw.
Thom Mushi.
Alifafanua kuwa mwili wa marehemu
utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi
yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha
Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Mtandao huu unatoa pole kwa
familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick
Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.
RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU – JUNIOR NATIONAL BASKET ASSOCIATION (JR.NBA)
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu
bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya
mitoano Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana
kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya
mpira wa kikapu kwa vijana, katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu
ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar
es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es
Salaam.
Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu
ya mashabiki wa Mpira wa kikapu walio fika katika uzinduzi wa Ligi
ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment