Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawane.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawane Amewasimamisha kazi
wakurugenzi wa nne kwa tuhuma za kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka
katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe
hati safi huku Halmashauri hizi Zikiwa na Ufisadi .
Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni
Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally
Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara na Abdalla Mfaume wa
Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
Pia,Waziri Simbachawene
amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya Bi
Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka
ikiwa ni pamoja na kuwatumia Watoto wake katika shuguli za halmashauri
na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Simbachawane pia
ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya Mkaguzi
wa Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa
wakurugenzi hao ili Watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku
zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo
mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao
wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake
Akibainisha makosa ya kila
mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Misenyi, Bi Chitundu alimwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato
atoe rushwa ya Milioni tatu kwa Maafisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la
kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo huku akijua ni kosa
kisheria. Watumishi wa wa ofisi ya CAG waliopokea pesa hizo ni Stevin
Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
Katika Halmashauri ya Nanyumbu,
Simbachawene amesema kuwa tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake Bwana
Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa
walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano afisa wa ofisi ya CAG kwa
lengo la kutoa hati safi
Waziri Simbachawene amesema mwezi
Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe Mkoani Geita
Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16 maafisa
wakaguzi wa ofisi ya CAG ili wafiche ufisadi walioubaini
Amesema katika Halmashauri hiyo pia
kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya Mishahara hewa
pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi
No comments:
Post a Comment