Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwasili eneo la tukio
kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati
ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi.
Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akiwahutubia
Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais,
Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu,
Bi. Joyce Fissoo (kushoto) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni
waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na
Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25
Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Uchaguzi wakitoa
maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu
wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF).
Viongozi wa Uchaguzi wakitoa
maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu
wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF).
Baadhi ya Wasanii toka vikundi
mbalimbali katika baadhi ya mikoa wakifuatilia kwa makini zoezi la
upigaji kura pamoja na sera na vipaumbele vya Wagombea wa ngazi
mbalimbali wakati wa uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe
wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25
Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia) akihitimisha ukomo wa
Serikali yake ya Shirikisho hilo kabla ya upigaji kura kuanza siku hiyo
ya 25 Februari, 2016.
Na Tabu Mullah
Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya
Filamu nchini inakua kwa kasi na kuleta manufaa kwa wasanii, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewahakikishia
wasanii juu ya kupatikana kwa Sera ya filamu ili kuleta matokeo chanya
ya katika kazi zao.
Mhe. Nnauye ameyasema hayo jana
jijini Dar es Salaam wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la
Filamu Tanzania (TAFF) ambapo ameahidi kushirikiana na Shirikisho hilo
katika nyanja mbalimbali na kuwataka wanachama kuchagua viongozi
wawajibikaji watakaoweza kusimamia Katiba kwa maslahi ya wote.
“Chagueni viongozi wenye weledi,
wawajibikaji na wachapakazi ili mshirikiane nao katika kuleta maendeleo
kutokana na kazi zenu kitaifa na kimataifa”, alisema Mhe. Nnauye.
Aidha, Mhe. Nnauye ameahidi
kutatua tatizo la usambazaji wa kazi feki za filamu ulioenea kwa kasi
nchini ambapo amesema kwa kushirikiana na wadau wa filamu nchini yaani
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Filamu pamoja na COSOTA
watahakikisha kuwa, kazi ambayo haina ubora haingii sokoni.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo ameeleza kuwa, Serikali itasimamia
kwa umakini filamu za nchini kwa kutoa mafunzo kwa vijana na Shirikisho
ili waelewe majukumu yao na jinsi ya kufanya kazi kwa weledi.
Bi. Fissoo ameongeza kuwa nidhamu
katika kazi ni muhimu kwa wasanii kwa kuwa inaleta heshima kwao na kwa
Taifa, hivyo ni wajibu wa kila msanii kufuata maadili ili kuzalisha kazi
nzuri zitakazopata soko ndani na nje ya nchi.
“Kuwepo katika Vyama ni msingi
mkubwa wa mafanikio, fuateni Katiba, tafuteni vipaumbele katika kazi
zenu na pia zingatieni muda kwa kila mtakalofanya, naamini
mtafanikiwa’’, alisema Bi. Fissoo.
Shirikisho la Filamu Tanzania
lilifanya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais na wajumbe kumi wa Bodi
Februari 25 mwaka huu, ambapo Bw. Simon Mwakifwamba alitetea nafasi
yake ya kiti cha Urais wa Shirikisho hilo kwa muhula wa miaka mine
(2016-2020) na Bw. Deo Sanga kuwa makamu wa Rais.
No comments:
Post a Comment