Dar es Salaam.
Na Kalonga Kasati
Shirika lisilo la kiserikali la
Tanzania Feminist and Youth Change Organization (TAFEYOCO) limemuomba
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha utaratibu
wa kukutana na vijana ili kujadiliana mambo mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti
wa Shirika hilo Bw. Elvis Makumbo alipokuwa akizungumza na waandishi
habari jijini Dar es Salaam katika mkutano uliyolenga kumpongeza
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya
katika siku mia moja za uongozi wake.
“Vijana kwa sasa katika taifa ni
wengi na ndiyo wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika nchi na nguvu kazi
ya Taifa na wanachangamoto nyingi hivyo Mheshimiwa Rais akijaribu
kukutana nao nakuwasikiliza matatizo yao itasaidia kuleta mafanikio
katika nchi na kujua nini kifanyike kuleta maendeleo katika Taifa,”
alisema Bw. Makumbo.
Ameleza kuwa, Mheshimiwa Rais
ameonyesha moyo wadhati wa kuwatumikia wananchi kwa kuwawajibisha watu
wote walionekana wakitumia vibaya madaraka yao na kufanya ubadhirifu wa
pesa za umma kinyume na taratibu za kiutumishi wa umma.
Mbali na hayo Bw.Makumbo
amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria kuanzisha mfumo au taasisi
itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni namna gani mali hizo
amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao tumia fedha za
serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea utajiri
mkubwa usiyolingana na kipato chao.
Mwenyekiti huyo aliendelea
kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi kuzingozea nguvu taasisi za Serikali ili
kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji mfano wa Taasisi hizo ni TAKUKURU
na nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali Yenye tija kwa Taifa.
Shirika hilo limesema Kauli Mbiu
ya Mheshimiwa Rais ya Hapa Kazi Tu imeongeza hari kubwa ya utendaji kwa
wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika ikiwemo kwa watu wa sekta binafsi na
taasisi
Prof Elisante Ole Gabriel akutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TSN
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kulia)
akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya
Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) kuhusu changamoto
mbalimbali za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwa katibu
mkuu ni Prof Moses Warioba ambaye ni mwenyekiti wa bodi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo
na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali
ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) Bw.Prof Moses Warioba
(kushoto).
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa
kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd
(TSN) wakimskiliza Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa kikao
cha kuzungumzia changamoto mbali mbali za kampuni hiyo.kutoka kulia ni
Dkt Consolatha Ishebabi,Dkt Evelyn Richard na Bw,Alfred Nchimbi.
Picha na Daudi Manongi-WHUSM
Kwaya mbili kusindikiza Tamasha la Pasaka
Na Mwandishi Wetu
KWAYA mbili za nyimbo za Injili
zimethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika
mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia Machi 26 hadi 28.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama tamasha hilo linaanza
Geita katika ukumbi wa Desire ambalo litafanyika Machi 26, Mwanza kwenye
uwanja wa CCM Kirumba litafanyika Machi 27 na Kahama Machi 28 kwenye
uwanja wa Taifa.
Msama alizitaja kwaya hizo
zinazotarajia kupanda jukwaani katika mikoa hiyo ni pamoja na AIC
Makongoro Vijana ya jijini Mwanza sambamba na Wakorintho Wapili ya
Mafinga ya Iringa.
Msama alitoa wito kwa wakazi wa
mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo Malengo yake
ni kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, yatima na wajane.
“Nawaomba wakazi wa mikoa ya
Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili tuwasaidie wenzetu wenye Uhitaji
maalum ambao ili wafikie malengo wanahitaji kutoka kwetu,” alisema
Msama.
Aidha Msama alisema bado
wanaendelea kufanya mawasiliano na waimbaji mbalimbali wa Tanzania ambao
kwa pamoja watafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
No comments:
Post a Comment