Baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi
wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na
kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti
mabalimbalai wamejitokeza na vielelezo vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo
ulivyoharibika
Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu
namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura
ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii ni fomu kutoka Kituo cha
Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo
halali kutokana na kukosa mhuri wa Tume ya uchaguzi Zanzibar. Msimamizi
wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid.
Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940
A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii ni fomu kutoka kituo cha
Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni namba 1926, fomu hii imepoteza
uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina mhuri wala jina la msimamizi wa
kituo.
B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii ni fomu kutoka katika kituo
cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618, Katika jimbo la Chumbuni namba
1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu imefutwa majina ya mawakala na
kupandikizwa majina mengine juu ya maandishi ya kivuli.
C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi mbili, fomu kutoka kiwanja
cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka jimbo la Chumbuni namba 1937,
fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina mhuri , maandishi ya meandikwa
tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi uya
mara moja. Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na
namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo
wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar
ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
D. Mihuri ya kughushi
Fomu ya pili ni kutoka jimbo la
Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali
kwasababu ina mhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.
E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC
alisema utata wa matokeo ulianza pale wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi
na kuiarifu Tume dhidi ya matendo yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC
Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na mabishano yakiendelea Mmoja wa
wagombea akaitisha wanahabari na kujitangaza ameshinda kwa matokeo
ambayo kila mmoja wetu alishangaa sana,
Ni kitendo cha aibu na Fedheha
kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara yake,sijui alitoa wapi Takwimu
ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea wawili tu,tena ukijumlisha asilimia
ni 100 inasikitisha sana,Shinikizo la kunitaka nimtangaze mshindi
kinyume na taratibu lilinifanya niubebe msalaba kusimamisha na kufuta
matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache za uthibitisho mwandishi haya
ndio tuliyakuta,Ni nusu ya uchaguzi wote kila jimbo ulichezewa
No comments:
Post a Comment