Na Tabu Mullah
JUMLA ya watoto 60 wenye umri
wa chini ya miaka mitano (5) kisiwani Pemba wamepatiwa kinga dhidi ya
ugonjwa wa kifua kifuu (Isonizid Prevent Therapy ) kwa kipindi cha
kuanzia janauri hadi disemba mwaka 2015 .
Akizungumza na mtandao huu
jana huko Ofisini kwake Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba , Ofisi wa
habari , elimu na mawasiliano kutoka Kitengo cha kifua kikuu Wizara ya
Pemba Hasnuu Fakih Hassan amesema kuwa watoto hao wale ambao wazazi wao
wanaugonjwa wa kifua kikuu .
Amesema kwamba matibabu hayo
ambayo yameanzishwa kwa watoto hao yamesaidia katika kuwakinga watoto
hado dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa huo ambapo hali zao zinaendelea
vyema .
Hasnuu alizidi kufafanua
kwamba watoto hao ishirini (20) wanatoka Mkoa wa Kaskazini Pemba na
arobaini (40) wanatoka Mkoa wa Kusini Pemba
“Tunao watoto zaidi
ya sitini walio chini ya umri wa miaka mitano , tumewaanzishi kinga
dhidi ya ugonjwa kifua kikuu Isonized Prevent Therapy , matibabu ambayo
yanawahusu watoto ambao wazazi wao wanaugonjwa wa kifua kikuu ”
alifahamisha .
Aidha alifahamisha kwamba
Kitengo hicho kimeweza kuwafikia wagonjwa wa kifua kikuu katika maeneo
wanayoishi , ambapo baada ya kuwapatia huduma wagonjwa pia wanatalaamu
hutumia muda huo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii .
Akizungumzia
maambukizi ya Ugonjwa huo Kisiwani Pemba Hasnuu alisema kwamba idadi ya
wagonjwa wa kifua kikuu imeongezeka kutokana na jamii kuwa na mwamko wa
kupima afya zao mara kwa mara .
Alisema kwama katika
kipindi cha oktoba hadi disemba Mkoa wa Kusini Pemba ulikuwa na wagonjwa
74 ambapo Mkoa wa Kaskazini Pemba ulipatikana wagonjwa 36 .
Alifahamisha kwamba
ongezeko la wazazi katika Mkoa wa Kusini Pemba imechangiwa na uwepo na
kituo cha maabara ya afya ya jamii , ambacho wamekuwa wakifanya kazi kwa
ushirikiano wa karibu .
“Unaweza kushangaa
kuona kwamba Idadi ni kubwa Mkoa wa Kusini Pemba , hii ni kutokana na
uwepo na maabara ya afya ya jamii ambayo imekuwa ikishirikiana nasi
katika kutoa Taaluma na uchunguzi wa maradhi hayo ” alifahamisha .
Hivyo ameitaka jamii
kufika haraka katika vituo vya afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi pindi
wanapobaini kwamba wanadalili ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu , na kuongeza
kwamba malengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 , Pemba kusiwepo na
mgonjwa wa kifua kikuu .
DK. KIGWANGALLA ADHURU KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA IRINGA
Eneo
la vijiji vya Pawaga linavyoonekana kwa picha za angani wakati wa Naibu
Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangallla amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kufika
katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli,
Tarafa ya Pawaga iliyopo Iringa vijijini Mkoani hapa ambapo mbali na
kutoa pole pia ameweza kutoa huduma za kitabibu kwa baadhi ya watu
waliozidiwa waliokuwa bado hawajaokolewa.
Awali
Dk. Kigwangalla alipodhuru kwa wananchi waliopo kwenye kambi ya muda
baada ya kunusurika na mafuriko hayo, aliwaeleza kuwa Serikali
itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega kwani Serikali ya “Hapa Kazi
Tu” haina ngoja ngoja ndio maana yeye ameweza kufika haraka kuakikisha
wananchi wapo salama na wanapatiwa huduma zote za msingi na za kijamii
ikiwemo matibabu na elimu ya kijikinga na milipuko ya magonjwa ikiwemo
magonjwa ya kipindupindu ambacho kimewakumba wananchi hao.
Dk.
Kigwangalla ameweza kufanya hilo baada ya Chopa iliyokuwa ikimtembeza
angani kufika katika maeneo yaliyozingirwa, alimuru rubani wake kushusha
chini na kisha kutoa msaada wa Haraka kwa akina mama na watoto
waliokuwa wamezingirwa kwenye moja ya maeneo hayo zaidi ya siku tatu
bila kuokolewa ambapo alitoa huduma na kisha Chopa hiyo iliwabeba hadi
katika eneo maalum waliopo wahanga wengine waliookolewa
Pia
Dk. Kigwangalla aliweza kutoa elimu na maelekezo mbalimbali kwa wahanga
hao kujiepusha na masuala ya kutumia mahitaji salama ilikuepukak
kipindupindu kisienee zaidi kwani hadi sasa eneo hilo limeweza
kupatikana wagonjwa wa ugonjwa huo zaidi ya 220 huku Hadi wanatembelea
katika kambi ya Mtakatifu Lucas iliyopo Pawaga, ilikuwa na wagonjwa
zaidi ya 40.
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa katika eneo lililokumbwa na mafuriko hayo kijiji cha Mbolimboli
No comments:
Post a Comment