Na Kalonga Kasati
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka
Dar es salaam (DAWASCO), imerejesha huduma ya Upatikanaji wa Maji
katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini jijini Dar es Salaam, pamoja na maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na
mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36 kuanzia siku ya Alhamisi
18/02/2015
Akizungumzia kurejea kwa huduma
hiyo, Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa
huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo mkoani
Pwani kwa sasa yameanza kwenda kwa wananchi, na maeneo mengi ya jiji
ambayo yalikosa huduma ya Maji kutokana na uzimwaji wa mtambo wa Ruvu
chini.
“Napenda kuwaambia wateja wetu
kuwa huduma ya Maji kwa sasa imerejea kwenye maeneo Mengi ya jiji baada
ya matengenezo kukamilika na mtambo kuwashwa siku ya Jumapili saa 9:30
alasiri” alisema Bi. Lyaro.
Alibainisha kuwa Kuna maeneo
mengine yatachelewa kupata Maji kwani mara nyingi kwa kitaalamu huwa
mtambo ukizimwa kwa zaidiya saa 24 ndani ya mabomba ya kupitisha Maji
hujaa hewa hivyo baadhi ya maeneo kazi ya utoaji hewa kwenye mabomba
unaendelea, hivyo tuwahakikishie wananchi kuwa huduma imerejea na
wataipata ndani ya muda tuliotarajia.
Awali, mtambo wa Ruvu Chini
ulizimwa ili kuwaruhusu wakandarasi kutoka kampuni ya sino Hydro na
mafundi kutoka DAWASCO kukarabati bomba la Maji lenye inchi 54
linalosafirisha Maji kutoka Bagamoyo mpaka matenki ya Chuo kikuu cha
ardhi, Bomba lililokuwa likivuja Maeneo ya Makongo Jeshini, na
kusababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kukosa Huduma ya
Maji, Mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko,
Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo mengine ni pamoja na
Maeneo ya Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo,
Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City
centre, Ilala,, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa
Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko
No comments:
Post a Comment