Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu
akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) na kuwaeleza kuhusu
Mafanikio waliyoyapata Katika Siku 100 za uongozi wa Rais John Pombe
Magufuli ikiwamo kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali
nchini, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Saalam, Kulia ni
Afisa Habari Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Lilian Lundo
NA Kalonga Kasati
Wakala wa Uchimbaji Visima na
Mabwawa (DDCA) wamefanikiwa kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu
mbalimbali nchini Katika Siku 100 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na
Mabwawa Bw. Egwaga Nungu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo
Jijini Dar es Salaam.
“Wakala wa Uchimbaji Visima na
Mabwawa (DDCA) katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi februari tumeweza
kufanikiwa kuchimba visima 52 zitakavyowezesha kupataikana kwa maji
safi kwa watanzania katika maeneo mbalimbali na pia wakala umefanikiwa
kuchimba mabwawa 3” Alisema Bw. Egwaga.
Akiongelea Matarajio na mipango
ya wakala Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Bw. Egwaga amesema kuwa wakala
unatarajia kuchimba visima 400, kupima wingi wa maji katika maeneo 420,
kusafisha visima 500, pumping installation visima 400 na kukarabati
visima 100.
YANGA v SIMBA KESHO TAIFA
Tiketi za mchezo wa watani wa
jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) kati ya Yanga SC dhidi ya
Simba SC Jumamosi, Februari 20, 2016 zimeanza kuuzwa leo Ijumaa saa 2
asubuhi leo asubuhi katika vituo 10 mbalimbali vilivyopo jijini Dar es
salaam.
Vituo vinavyotumika kuuza tiketi
za mchezo huo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom,
Uwanja wa Taifa Temeke, Mavuno House – Posta, Dar Live Mbagala,
Breakpoint – Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na
Kivukoni Ferry.
Kiingilio cha juu cha mchezo huo
ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000)
VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa
(Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Milango ya Uwanja wa Taifa
itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe
ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika maalumu ndiyo
yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara
ya Mandela na uwanja wa Uhuru.
Upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi
na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi
wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi,
mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.
Shirikisho linawaomba wapenzi,
wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari
ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la
kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.
Mchezo huo utachezeshwa na
mwaamuzi Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na mwamuzi Josephat Bulali
(Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji
za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo
atakua Khalid Bitebo (Mwanza).
SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE MAREKANI
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani
(Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe
19 Febuari, 2016.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
wakizungumza na Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Sweden waliotembelea
Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment