Baraza
la ushauri la chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii (VHTTI) limetakiwa
kuhakikisha linaandaa wanafunzi vyema na wenye viwango vya kimataifa
ili kukabiliana na ushindani mkubwa ulioko katika sekta ya hoteli na
utalii duniani.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa wakati akizindua
baraza hilo jana ndani ya chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI
kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha .
Alisema
kuwa kutokana na changamoto kubwa ya hoteli zetu kuajiri watu kutoka
nje ya nchi ikiwemo kenya na hata nchi za bara ya ulaya kwa kile
kinachodaiwa vijana wazawa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na
sekta ya hoteli na utalii hivyo ni wajibu wao kuakikisha wanafundisha
wanafunzi ili waweze kuwa na elimu ya kiwango cha kimataifa .
Alibainisha
kuwa wanatakiwa wahakikishe wanachuo ambao wanawafundisha wanakuwa na
sifa zinazotakiwa huku akiongeza kuwa mafunzo wanayofundishwa yawe bora
yanayokidhi maitaji ya ajira .
Aidha
alisema kuwa iwapo watawafundisha wanafunzi hao vyema na kuwapa elimu
inayoitajika kuoendana na soko hii itawasaida kupunguza kwa kiasi
kikubwa tatizo la ajira kwani wanafunzi hawa pindi watakapo maliza elimu
yao itakuwa raisi kupata kazi kulingana na elimu walikuwa nayo.
''pia
napenda kuwashauri kuanzisha lunga zote za kimataifa katika chuo chenu
ili mwanafunzi anaetoka katika chuo hichi aweze kuwasiliana na mgeni
yeyote ambaye atakuja kutoka katika nchi yoyote huko kazini kwake
anapoenda kwakweli inachekesha sana kuona mgeni anakuja alafu mwanafunzi
anaanza kuongea lunga mfano ya kingereza kwa kukosea kosea au anaongea
frechi kwa kukose kosea''alisema munasa
Kwa upande wa Mkurugenzi
wa
Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kuwa wao kama Veta wameamua
kuanzisha chuo hichi cha hoteli na utalii ili kuweza kupunguza tatizo
la ajira ambalo linaendelea kwa vijana wengi.
Aliesema
kuwa chuo hichi kitatoa mafunzo ya hoteli na utalii katika ngazi ya
cheti na shahada kwa wasimamizi na waangalizi wa hoteli zetu.
Naye
mkuu wa chuo hicho Flora Hakika alisema kuwa wataji taidi
kuwafundisha wanafunzi vyema na wataanza kwa kuaandaa mitaala mipya
huku wakiwa wanaangalia zaidi jinsi wenzetu wa nchi za nje wanavyo
fanya pia watajitaidi kulenga kupata maitaji ya soko linavyoitaji ili
kuweza kuinua zaidi utendaji kazi wa vijana wa kitanzania
No comments:
Post a Comment