Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Baba Askofu Dkt
Fredrick Shoo akitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Isalia Elinewinga
wakati wa shughuli ya Mazishi iliyofanyika kijiji cha Losaa Masama
Magharibi wilayani Hai.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Isalia Elinewinga.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa Waziri wa
Elimu wa zamani ,Isalia Elinewinga aliyezikwa nyumbani kwake kijiji cha
Losaa wilaya ya Hai.
Baadhi ya waombolezaji walifika kwenye msiba huo.
Waziri
wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ,Prof Joyce Ndalichako
akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala wakiwa katika mazishi
ya Marehemu Isalia Elinewinga.nyuma yao ni Mkuu wa wilaya ya
Hai,Anthony Mtaka.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe pamoja na Mkewe Dkt Lilian Mtei wakiwa katika mazishi ya Marehemu Elinewinga.
Familia ya Marehemu Elinewinga wakiwa wenye huzuni kando ya Jeneza lenye Mwili wa Mpendwa Baba yao mzee Isalia Elinewinga.
Siku 100 Za JPM Usafi Wapewa kipaumbele.
Na Kalonga Kasati
Mnamo tarehe 5 Novemba 2015
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishuhudia Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akiapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano katika sherehe
zilizofanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Huu ndio ulikuwa
mwanzo mpya wa Tanzania ya uwajibikaji na maendeleo ya mtu wa hali ya
chini ambayo watanzania wengi walisubiri kwa muda mrefu vizazi na vizazi
kuiona.
Siku 100 tangu Rais wa awamu ya
tano aiingie madarakani mambo mengi yametiliwa mkazo kama vile Elimu,
Afya, Biashara, Viwanda,Kilimo,Ufugaji,Uvuvi na mengine mengi ambayo
serikali imeamua kuyaangalia kiundani zaidi ili kufanikisha azma yake ya
kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Katika makala hii tuangalie jinsi
uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano katika siku 100 ulivyojikita
kuimarisha usafi wa mazingira ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
yanayotokea mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini kwa kuhamasisha
usafi katika maeneo hayo. Hapa tunamsikia Mhe. Rais John Pombe Magufuli
akisema, “Hatuwezi kufanya sherehe huku watu wetu bado wanakufa kwa
ugonjwa wa kipindupindu ambao unatokana na uchafu, badala yake nchi
nzima tufanye usafi siku hiyo”.
Kwa kuliona hilo kwa niaba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli,
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza rasmi kuwa siku ya
tarehe 9 Desemba mwaka 2015, itakuwa ni siku ya uhuru na kazi na
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika kuwa yatafanyika kwa
watu kufanya usafi katika maeneo yao siku hiyo, ikiwa ni jitihada za
Serikali kuimarisha usafi na kupambana na magonjwa ya mlipuko kama vile
Kipindupindu.
Kero ya uchafu ilimfanya Mhe.
Rais kufanya tendo la kihistoria ambalo halijawahi kufanyika kwa
takribani zaidi ya nusu karne ya uhai wa Tanzania. Tukio hili ni
kuhamisha maadhimisho tuliozoea ya kuona gwaride la vikosi vya ulinzi na
usalama pamoja na halaiki na lakini sasa tunashuhudia machepe, troli,
ndoo, fyekeo na zana nyinginezo za usafi zikitumika siku hiyo. Ama kweli
Dr. Magufuli ni kiongozi mwenye uthubutu.
Naibu Waziri Wa Afya DK. Kigwangalla Aupa Siku 90 Uongozi Wa Hospitali Ya Mkoa Wa Njombe
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akikagua mahabara ya hospitali hiyo ambayo alikutana na matatizo mbalimbali ikiwemo mashine na vifaa kutotumika ipasavyo na kuagiza uongozi wa kufanya maboresho ndani ya miezi mitatu huku akiahidi kuifungia endapo itashindwa kutekeleza maagizo hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akiangalia moja ya maeneo ya wodi hizo ambapo alikuta hali ya uchafu pamoja na kuwa na mpangilio mbovu wa namna ya utoaji wa huduma.
Dk. Kigwangalla akitoa maelezo kwa Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Njombe-Kibena, Dk. Samwel Mgema wakati wa maagizo hayo ndani ya siku 90 na endapo hawatafanya utekelezaji ataichukuia hatua ya kuifungia.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akielekea kwenye baadhi ya majengo ya hospitali hiyo wakati wa ukaguzi huo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akikagua eneo la kutolea huduma ikiwemo wagonjwa Wanaoingia kumuonna Daktari.
Uongozi
wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90
kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo
itafungwa.
Kauli
hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na
viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na na Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.
Dkt.
Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali,
vituo vya afya na zahati ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio
waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.
Miongoni
mwa maagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na
vya maabara za kisasa, dawa za kutosha, kuaanza malipo ya mtandao.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina
baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo ni muhimu kwa uchunguzi wa magonjwa
mbalimbali, ikiwemo mashine ya CT-Scan na kuwepo kwa vifaa vibovu
ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovu wa ukusanyaji taka
ngumu na nyepesi.
“Sijaridhishwa
na uendeshaji wa hospitali hii na utoaji wa huduma zinazotolewaa
ninakuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, John Luanda kurekebisha mapungufu
yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikikuta huduma bado hairidhishi
nitakifunga kituo.,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Aliongeza kuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa ya Serikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu.
Dkt.
Kigwangalla aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na
mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo na
kuuwasilisha kwake.
Aliutaka uongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo.
No comments:
Post a Comment