Meza kuu ikifuatilia kwa makini
yanayojiri katika kikao cha uzinduzi wa Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa
elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
akieleza jambo wakati wa uzinduzi Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu
na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
Bi. Susan Rutledge, Mtafiti na
Mshauri wa masuala ya fedha, akieleza umuhimu wa elimu ya masuala ya
fedha kuelekezwa kwa wananchi.
Na Kalonga Kasati
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa
kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Kifedha Tanzania (FSDT),
imezindua Mwongozo wa taifa wenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu elimu
ya mambo ya fedha kwa wananchi.
Uelimishwaji wa wananchi kuhusu
mambo ya fedha utatekelezwa kupitia “Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa
elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
Gavana Prof. Beno Ndulu
ameuzindua rasmi mwongozo huu ambao utajikita katika kutatua changamoto
zilizobainishwa katika utafiti uliopima uelewa wa mambo ya fedha kwa
watu wazima nchini Tanzania. Utafiti huu unaitwa “Uwezo wa Kifedha
Tanzania” wa mwaka 2014.
Utafiti huo umebainisha kuwa
watanzania wengi hawana elimu na ujuzi mahususi wa masuala ya mambo ya
fedha kwa ujumla, hivyo kuwanyima fursa ya kutumia huduma za kifedha kwa
faida yao.
Katika utafiti huo imeonyeshwa
kuwa upatikanaji wa huduma za fedha umekuwa na changamoto katika maeneo
mengi huku zile zitolewazo kwa njia ya mitandao bado hazikidhi matarajio
ingawa zinawafikia wateja wengi kwa sasa.
Sambamba na hilo kumekuwa na
uhaba wa nyenzo na miundombinu ya kuhifadhi na kufikisha taarifa za
fedha kwa watumiaji wa huduma hizo kwa kuzingatia namna sahihi ya kutoa
taarifa, kuwaelimisha na kuwalinda.
Kutokana na utafiti wa “Uwezo wa
Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014 wananchi kutoka makundi mbalimbali
katika jamii hawana ujuzi wa hesabu za kawaida ambao ndiyo msingi mkuu
katika nadharia ya masuala yahusuyo mambo ya fedha.
Elimu msingi katika masuala ya
fedha umekuwa kikwazo kwa waliowengi hasa katika uandaaji wa bajeti,
kutunza kumbukumbu ya matumizi, kupanga fedha kwa matumizi
yasiyotegemewa ama ya ziada na muhimu zaidi kutunza kiasi kwa ajili ya
matumizi ya uzeeni (baada ya kustaafu).
Inaonekana kuwa upatikanaji wa
taarifa za masuala ya fedha hutegemea zaidi vyombo vya habari kama
redio, televisheni na magazeti lakini vyombo hivi kwa sehemu kubwa,
hufikisha zaidi taarifa Za biashara na masoko kuliko ambavyo
vinaelimisha jamii kuhusu matumizi na Upangaji wa mapato yao.
“Haya ndiyo masuala mahususi
ambayo mwongozo huu wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha unalenga
kushughulika nayo,” alisema Prof Ndulu.
Pamoja na kuwepo ongezeko la
upatikanaji wa huduma za kifedha, mpaka asilimia 58 mwaka 2013 kutoka
kiwango cha asilimia 17 mwaka 2009, miongoni mwa watu wazima nchini,
bado Mwongozo huu ni muhimu ili kuleta mfumo imara wa sekta ya fedha na
Zaidi sana ili kuleta ustawi wa maisha ya watanzania kwa ujumla.
Prof. Ndulu anasema kutatua
changamoto za kielimu kwa ujumla na hususan elimu ya huduma za Fedha
italiwezesha taifa kuwa katika mwelekeo mzuri wa kukabiliana na
umasikini na kufikia malengo ya kukuza uchumi.
“Tunapaswa kujiuliza: ni kwa
namna gani wananchi hasa wale masikini na wasiokuwa na elimu za kifedha
za wanapambana kuendeleza biashara zao katika mazingira ya soko huria
na lenye ushindani kila uchwao” alisisitiza Prof. Ndulu.
Hivyo, mwongozo huu utahakikisha
watanzania wapata elimu sahihi na ya uhakika ya huduma za kifedha pamoja
na njia anazoweza nazo kujilinda katika ushindani huu.
Vilevile mwongozo huu umeundwa
ili kutatua changamoto za kifedha zinazohusiana na maamuzi Miongoni mwa
watumiaji wa huduma hizi na kuwa jumuishi na wenye tija kwa jamii na
taifa kwa ujumla.
Mwongozo wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha umeandaliwa kwa kujumisha washikadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Unabainisha changamoto
zinazohusuana na uwezo wa kifedha ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uwepo
wa elimu ya fedha. Pia, unatoa taratibu wakufanikisha utekelezaji wa
elimu ya fedha, na mwongozo wa kitaifa wa kuratibu elimu ya fedha
nchini.
Lengo la mwongozo wa elimu ya huduma za fedha ni kuwa na wananchi na kaya zenye uwezo kifedha nchini.
Kombe La Shirikisho Kuendelea Wiki Hii
Michuano ya Kombe la Shirikisho
(Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa
nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini.
Jumatano Februari 24, 2016
kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young Africans
watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:30
jioni.
Michezo miwili itachezwa siku ya
Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa
Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwakaribisha wakata
miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi Februari 27, Mwadui FC
watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui
Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza
dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo.
Mzunguko huo wa nne utakamilika
siku ya Jumapili ambapo, Simba SC watawakaribisha Singida United katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja
wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita
Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
NB: Rais wa TFF, Jamal Malinzi
kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi, ataongea na waandishi wa habari
katika Ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.
DK Shein Amezungumza Na UVCCM Mkoa Wa Mjini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa
Mjini kichama leo katika ukumbi wa CCM Amani Mjini Unguja na kuwataka
Vijana kulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar,ikiwa ni katika hatua
za uimarishaji wa Chama cha Mapinduzi,[Picha na Ikulu.]
Makamu Wa Rais Akutana Na Ujumbe Wa Watu Wa China Na Mwenyekiti Wa Shell Deep
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa
kampuni ya Gezhouba kutoka China kuhusu masuala ya uwekezaji. Kushoto ni
kiongozi wa msafara huo Mhandisi Hu pend.
No comments:
Post a Comment