Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi
ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza
upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa
Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest
Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi
ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu
kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo,
Lilian Mapfa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizarani hapo, Haji
Janabi. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba,
anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Avelin Momburi na
Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha
kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA pamoja na Wakuu wa
Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) na
kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam
leo. Wa pili kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, na anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza jambo katika
kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake,
kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya NIDA na Wizara
kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara
hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tano kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na
Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh.
Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo
la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na
Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh.
Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo
la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira. Wengine
katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makumu wa Rais Bw. Mbarak
Abdulwakil na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Barthlomew Jungu.
Badilisheni Sera zenu Muandike Habari chanya kwa watu wenye Ulemavu: Dkt Possi
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi akizungumza na Wamiliki na wahariri
wa vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dare s salaam.
Mhadhiri toka Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Shule ya Uandishi wa Habari Dkt Harub Riyoba (katikati)
akimsikiliza Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt
Abdallah Possi alipokutana na Wamiliki wa Vyombo vya habri kulia ni
Mkurugenzi wa Uendeshaji toka Azam Media Yahya Mohamed na kushoto ni
Meneja wa Uendeshaji toka Sahara Media Steve Diallo.
Na Kalonga Kasati
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari
nchini kuwa na sera katika vyombo vyao inayojumuisha uandishi wa habari
chanya kwa watu wenye ulemavu.
Akitoa agizo hilo mbele ya wamiliki wa
vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi
amesema habari nyingi zinazohusu watu wenye ulemavu ni za kuwanyanyapaa
na kuonesha kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo chanya.
“Wekeni kipengele katika sera zenu
kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya
jumuiya katika maisha ya kila siku ya wanadamu,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya
habari vikiwa na sera iliyowazi na kuitekeleza, watu watabadilika na
kupata taarifa nzuri za watu wenye ulemavu.
Dkt. Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha zenye chembechembe za kunyanyapaa.
Amesema kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.
Amesema, “Serikali kwa kutumia Sheria ya
Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inaandaa tangazo kuvikumbusha
vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi
muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu.”
Aidha Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa
vyombo vya habari kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu kwani Sheria
inaagiza lazima chombo chochote chenye wafanyakazi zaidi ya 20, angalau
mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye ulemavu.
Kwa upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu habari chanya za watu wenye ulemavu.
Hata hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu
Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera pamoja na kuwa na wataalam wa kutafsiri
habari na vipindi muhimu kwa watu wenye ulemavu ni jambo zuri, lakini
wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.
No comments:
Post a Comment