Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa
Raia
wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama
rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.katibu huyo mkuu wa Fifa
alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya
mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein
alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa
kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza
kupigwa mjini Zurich.
Infantino akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FIFA
Raundi ya kwanza ya upigaji
kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa mojaWingi wowote wa
kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa
unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri
wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland
,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza
shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya
kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha
miaka sita .
Infantino akiwahutubia wajumbe
Baada ya kutangazwa mshindi,
Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea
kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa’
MWANAMUZIKI WA ZAMANI KASSIM MAPILI AZIKWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiweka udogo kwenye kaburi la Mwanamuziki
mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili, wakati wa mazishi
yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Mwili wa mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili ukiwasili kwenye makabuli ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Mwili wa mwanamziki mkongwe hapa nchini, Kassim Said Mapili
ukiwekwa katika kabuli wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makabuli
ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Waombolezaji waliofika kumsindikiza kwenye nyumba ya milele Mzee Kassim Said Mapili, wakipata mawaidha baada ya mazishi.
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipeana mikono na
mwanamuziki mkongwe Mjusi Semboja huku akiongea na Mzee Makassy na
wanamuziki wengine
Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongea na mchambuzi wa
muziki wa dansi mahiri Zomboko na mdau wa muziki Hassan.
MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini
wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini
wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya
kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya
kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es
salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAWAZIRI WOTE WAJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI
Na Kalonga Kasati
Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao
hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12
leo jioni limetekelezwa.
Waziri Mkuu amepokea barua kutoka
kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji
(Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote
wametekeleza agizo hilo.
“Hadi kufikia saa 9.30 leo
alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha
fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.
Rais Magufuli leo
asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la
Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa
12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na
Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar
es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa
amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.
No comments:
Post a Comment