KAMPUNI YA KUOSHA MAGARI KWA KUTUMIA MVUKE YA SHINE ECO WASH LIMITED YATUA JIJINI DAR ES SALAAM
Baadhi ya magari ya wateja
yakiendelea kuoshwa katika kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye
makazi yake Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wafanyakazi katika
kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye makazi yake Mlimani City jijini
Dar es Salaam akiendelea na kazi ya uoshaji.
Kazi ya uoshaji wa magari ikiendelea katika kampuni hiyo
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Tabu Mullah
Kampuni inayojishughulisha na uoshaji wa magari kwa njia ya mvuke imeanza kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mahojiano
maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Elia Richard Moshi alisema
kuwa lengo la kampuni hiyo ni kutoa huduma ya kipekee kwa kuosha
magari kwa kutumia mvuke ni kuzuia uharibifu wa mazingira.
Akielezea utofauti wa huduma hiyo na huduma zingine Moshi alisema kuwa kampuni inatumia maji yasiyo na kemikali ya aina yoyote (distilled water) ambapo gari moja huoshwa kwa kutumia lita tatu hadi tano za maji kwa njia ya mvuke ijulikanayo kama steaming.
Alisema kuwa awali alifanya
utafiti na kubaini kuwa kwa kawaida gari moja huoshwa kwa kutumia
lita 85 hadi 125 hali inayochochea upotevu wa maji na uharibifu wa
mazingira, hali iliyopelekea yeye kubuni wazo la kuanzisha kampuni ya
kuosha magari kwa kutumia maji kidogo yasiyo na kemikali kwa kutumia
mashine maaluum.
Aliongeza kuwa huduma nyingine wanazotoa kama kampuni ni pamoja na kung’arisha magari kwa nje (body polishing) ili kuondoa mikwaruzo na madoa sugu, kung’arisha gari kwa ndani (interior polishing) na kusafisha engine bila kutumia maji.
“Unajua unapotumia maji kuosha engine
ya gari hususan kwa magari ya kisasa, unaharibu gari, hivyo
tunaosha bila kutumia maji kwa kutumia mashine maalum pamoja na
kung’arisha,”alifafanua Moshi.
Aliendelea kufafanua kuwa
watumiaji wa magari wanashauriwa kuosha magari kwa kutumia mvuke
angalau mara moja kwa mwezi na kuwataka wamiliki wote waishio jijini Dar
es salaam kupeleka magari yao katika kampuni yake yenye makazi yake
katika viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuoshwa.
Akielezea malengo ya kampuni yake
katika kusambaza huduma kwa wafanyakazi waliopo maofisini, Moshi
alisema kuwa kampuni ina mashine maalum (mobile machine) zenye uwezo wa kufanya kazi sehemu yoyote ambapo wateja wanaweza kusogezewa huduma kwenye maofisi yao.
“Wateja waliopo maofisini wana uwezo wa kujiorodhesha na sisi kama kampuni kuwafuata maofisini na kuwaoshea magari yao kwenye parking zao huku wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na kwa usalama zaidi” alifafanua.
Hata hivyo aliongeza kuwa kampuni
ina mpango wa kufungua matawi jijini Dar es Salaam na katika mikoa ya
Arusha, Dodoma na Kilimanjaro na mingine kwa siku za usoni
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wakazi wa jijini Dar es Salaam kuhusu huduma ya kampuni hiyo walisema
kuwa wameanza kunufaika na huduma hiyo na kufurahishwa na utendaji kazi
wa kampuni hiyo.
Salum Salehe mkazi wa Masaki
jijini Dar es salaam alisema kuwa tangu ameanza kutumia huduma hiyo,
gari yake imekuwa ikionekana mpya kila kukicha na kuwataka watumiaji
wengine wa magari kutumia kampuni hiyo katika uoshaji wa magari yao.
Alisema kuwa mbali na mwonekano
wa gari yake kuimarika, kampuni hiyo imekuwa ikokoa muda mwingi kwani
anakabidhi gari kwa kampuni na kuendelea na majukumu yake kama kawaida
ambapo hufuata baadaye baada ya kazi ya uoshaji kukamilika.
Naye Victor Moshi mkazi wa
Kinondoni aliongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiwasiliana na wateja
wake kwa njia ya sms kwa ajili ya kuwashauri juu ya utunzaji wa magari
yao jambo ambalo ni jema.
WIZARA YALAANI MAUAJI YA MTOTO MARIAM DEOGRATIUS (4) ALIYEBAKWA NA KUUAWA ENEO LA MAKOKO, MUSOMA MKOANI MARA
Wizara inalaani vikali tukio la
kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4,
ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko,
Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii.
Wizara imesikitishwa na mazingira
ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa
kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa
na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji
mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi.
Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya
jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi.
Wizara inaamini kuwa, Mamlaka
zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara
hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya
vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa
fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
Wizara inatoa pole kwa wazazi,
ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo
na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
- S. Nkinga
KATIBU MKUU
25/02/2016
No comments:
Post a Comment