Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akisisitiza jambo
eneo la Kiluvya wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja
mwishoni mwa wiki kukagua shughuli za upanuzi mitambo Ruvu Juu na Ruvu
Chini, ulazaji wa bomba na ukarabati wa matanki kazi inayosimamiwa na
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA).
Baadhi ya mitambo mipya ya
kusafirishia maji kutoka chanzo cha maji cha Ruvu Juu eneo la Ruvu
Darajani kuelekea sehemu ya kusafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwa eneo la Jengo jipya
ilipo mitambo mipya iliyopo chanzo cha maji cha Ruvu Juu eneo la Ruvu
Darajani kuelekea sehemu ya kusafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji.
Na Tabu Mullah
Nimeridhishwa na kasi ya ulazaji
wa mabomba ya maji kutoka vyanzo vya Ruvu Chini na Ruvu Juu, ukarabati
wa matanki na ujenzi wa matanki mapya ya maji kutokana na eneo dogo
lililobakia ili kukamilisha miradi na kuwapatia maji ya uhakika
wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
Kazi ya ulazaji wa bomba la maji
hadi matanki yaliyopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam,
lenye urefu wa km 55.5 ambalo linasafirisha maji kutoka chanzo cha
Mtambo wa Ruvu Chini Bagamoyo mkoani Pwani imebakia km 1.1 ili
kuwapatia maji ya uhakika wakazi wa mikoa hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo alitoa kauli hiyo alipofanya
ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa wiki kukagua shughuli za
upanuzi Mitambo Ruvu Juu na Ruvu Chini, ulazaji wa mabomba na ukarabati
wa matanki kazi ambayo inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka Dar es Salaam (DAWASA).
“Jukumu la kuwapatia maji ya
uhakia wakazi wa mikoa ya Pwani na Dar es salaam katika miradi yote
miwili ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ni kuhakikisha ukarabati wa matanki ya
Kimara, ujenzi wa Tanki jipya Kibamba na ulazaji wa bomba unakamilika
kwa wakati” alisema Mhandisi Kalobelo.
Akifanya majumuisho baada ya
kukagua kazi ya ukarabati wa matanki ya Kimara, ujenzi wa tanki jipya
Kibamba na ulazaji wa bomba Ruvu Juu yanasukumwa kutoka chanzo cha maji
cha Ruvu Darajani kupitia kwenye bomba hadi matanki yaliyopo Kimara,
lenye urefu wa km 51 Mhandisi Kalobelo amemtahadharisha Mhandisi Mural
Mohan wa kampuni ya Megha kutoka nchini India inyofanya kazi katika
mradi huo kuwa kulingana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa nchini Mwaka huu kuna mvua nyingi, hivyo aongeze nguvu na kasi ya kulaza
mabomba hasa maeneo ya mabondeni ili akamilishe mradi huo ndani ya mwezi
wa tatu.
Mhandisi Kalobelo ameridhishwa na
kasi ya makandarasi wanaojenga mradi huo baada ya kutembelea ukarabati
wa matanki ya Kimara, ujenzi wa tanki jipya eneo la Kibamba, ulazaji wa Bomba eneo la Kiluvya na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu eneo la Ruvu
Darajani.
Kwa upande wake Mhandisi Mural
Mohan wa kampuni ya Megha kutoka nchini India Amemhakikishia Mhandisi
Kalobelo kuwa watafanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo Ndani
ya muda uliopangwa ili kuwapatia wananchi wa mikoa ya Dar es salaama na
Pwani huduma ya maji ya uhakika na kuondoa kero ya upatikanaji wa maji
iliyowasumbua wananchi hao kwa muda mrefu.
Aidha, baada ya kujionea kazi
iliyofanywa kwenye mradi wa Ruvu Juu, Mhandisi Kalobelo Alielekea kwenye
chanzo cha maji cha Ruvu Chini kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa
Pwani ambapo alijionea mitambo mipya inavyofanya kazi ya kusafisha maji
kabla ya kusafirishwa kwenda kwa watumiaji ambao ni wakazi wa mikoa ya
Dar esa salaam na Pwani na kuhitimisha Ziara yake eneo la Mbezi Beach
ambapo kimebakia kipande cha km 1.1 kukamilisha kazi nzima ya ulazaji wa
bomba.
Aidha, Mhandisi Kalobelo amewasihi wakazi wa maeneo yote ilipo au ilipopita miundombinu ya maji wailinde na kuitunza.
Pia ameziagiza mamlaka
zinazohusika na ulinzi kufanya utaratibu wa kuwa na ulizi wa uhakika ili Miradi hiyo inapozinduliwa na mitambo kuwashwa kuwe na uhakika wa
miundombinu ya maji kuwa salama kwa kuwa uwekezaji uliofanyika umetumia
ghrama kubwa za walipa kodi na washirika wengine wa maendeleo wenye nia
njema ya kuboresha huduma za jamii ikiwemo maji.
Kwa upande wao Mkurugenzi wa
Huduma za Ufundi (DAWASA) Romanus Mwang’ingo na Afisa Msimamizi wa Kituo
cha uzalishaji maji Ruvu Chini kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka
Dar es Salaam (DAWASCO) Tumaini Ndosi wamesema kuwa wako bega kwa bega
na wakandarasi Wanaofanya kazi katika miradi yote miwili ili kutekeleza
ahadi na azma ya vingonzi nchi ya kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es
salaam na mkoa Pwani maji ya uhakika waweze kujiletea maendeleo yao
ikizingatiwa hakuna maisha bila maji.
Maeneo ambayo wakazi wake
watanufaika na huduma ya maji ni kuanzia maeneo ya uwekezaji (EPZ)
Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.
Maeneo mengine yatakayonufaika na
mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na
Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni,
Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini
wakati Mtambo wa Ruvu Juu Utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi,
Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo
lote la Tabata.
No comments:
Post a Comment