Manchester United watakutana na mahasimu wao wa jadi Liverpool katika hatua ya 16 bora katika Europa League.
Valencia, walio chini ya Gary Neville, watakutana na wapinzani wao katika La Liga Athletic Bilbao.

Mechi hizo zitachezwa Alhamisi tarehe 10 na 17 Machi.
Washindi wa ligi hiyo watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka ujao.
United, ambao hawajawahi kushinda Europa League, walilaza FC Midtjylland kwa jumla ya mabao 6-3.

Rashford alifungia Manchester United mabao mawili
Marcus Rashford alifunga mabao mawili mechi yake ya kwanza kabisa kuwachezea mechi ya marudiano ambayo United walishinda 5-1 usiku wa Alhamisi.
Liverpool chini ya Jurgen Klopp walisonga kwa kulaza Augsburg 1-0 kwa jumla, bao la pekee likifungwa na James Milner Alhamisi.
Klabu hiyo ilishinda kombe la zamani lililokuwa likijulikana kama Kombe la Uefa mara tatu 1973, 1976 na 2001.
Itakuwa mara ya kwanza kwa United na Liverpool kukutana ligi ya Ulaya.
Droo kamili ya Europa League hatua ya 16
- Shakhtar Donetsk v Anderlecht
- Basel v Sevilla
- Villarreal v Bayer Leverkusen
- Athletic Bilbao v Valencia
- Liverpool v Manchester United
- Sparta Prague v Lazio
- Borussia Dortmund v Tottenham
- Fenerbahce v Brag

No comments:
Post a Comment