Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mteule
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo
alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi mteule
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo
alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha,[Picha na Ikulu.]
Mpinzani wa Cheka awasili na kutema cheche, Amwita Cheka Babu
Bondia Mserbia anayeishi
Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Advanced
Security, Juma Ndambile (kushoto) na Promota Jay Msangi (kulia) katika
mkutano na waandishi wa habari jana. Ajetovic atapigana na Francis
Cheka Jumamosi kwenye viwanja vya leaders club kuwania mkanda wa uzito
wa Super Middle wa Mabara wa chama cha WBF
Bondia Mserbia anayeishi
Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
jana tayari kwa pambano lake la jumamosi dhidhi ya Franci Cheka. kushoto
ni Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile na kulia ni promota
Jay Msangi. Ajetovic atapigana na Francis Cheka Jumamosi kwenye viwanja
vya leaders club kuwania mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara wa
chama cha WBF.
Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile (katikati) akizungumza katika mkutano huo.
Na Mwandishi wetu
Bondia Geard Ajetovic amewasili
nchini na kumuita bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini ,Francis
“SMG” Cheka kuwa ni ‘babu’ na hawezi kupigwa na bondia huyo pamoja na
kupigana katika ardhi ya Tanzania.
Ajetovic alisema kuwa anamjua
Cheka kwani amemuona kwenye pambano lake dhidi ya Thomas Mashali na
kusema kuwa ‘amekwisha’ na kamwe si bondia wa kupambana naye.
Alisema kuwa Cheka amepigwa na
bondia ambaye si lolote wala chochote na atampiga kabla ya raundi ya
tano katika pambano hilo la ubingwa wa Mabara la uzito wa Super Middle
unaotambuliwa na chama cha WBF.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Advanced Security, Juma Ndambile aliwahakikishia mashabiki wa ngumi za
kulipwa nchini kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika bada ya
ujio wa Ajetovic.
Ndambile alisema kuwa maofisa
wa Chama cha WBF, ikiwa pamoja na Rais wake, Howard Goldberg na mwamuzi
wa pambano hilo ambao watawasili leo.
“Kama nilivyosema hapo awali,
dhamira kubwa ya kampuni ya Advanced Security in kuendeleza mchezo wa
ngumi za kulipwa nchini hasa kwa mabondia kufaidika na vipaji vyao na si
vinginevyo,”
“Ili kufikia lengo letu,
Advanced Security imeamua kuwashirikisha mabondia chipukizi katika
mapambano ya utangulizi. Mabondia hao chipukizi wanatarajia kutoa
changamoto kwa mabondia maarufu ambao pia watashiriki katika pambano
hilo,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa wameandaa mabondia
chipukizi ili kupamba siku hiyo. Alisema kuwa Mohamed Bakari atapambana
na Cosmas Cheka katika pambano la uzito wa feather la raundi nane (8)
huku Mohamed Matumla ataonyeshana kazi na Mustapha Dotto katika pambao
la uzito wa Light la raundi nane pia.
Bondia mkongwe na maarufu
nchini, Mada Maugo ataingia ulingoni kwa kupambana na bondia kutoka
Mbeya, Baraka Mwakansope baadala ya bondia Abdallah “Dulla Mbabe” Pazi
kama ilivyotangazwa awali.
Alisema kuwa pia siku hiyo,
bondia wa kike, Lulu Kayage atazichapa na bondia nyota kutoka mkoa wa
Mbeya, Mwamne Haji katika pambano la uzito wa fly lilillopangwa kuwa la
raundi sita.
Bodi ya Mikopo yatoa utaratibu wa kuwasilisha malalamiko
Meneja wa Habari , Elimu na
Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Omega Ngole
akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu utaratibu wa
kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kuhusu upatikanaji wa mikopo elimu
ya juu uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Na Kalonga Kasati
Dar es salaam
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) imetoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya
wanafunzi wanaopata mikopo katika taasisi za elimu ya juu nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano Omega Ngole alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kushughulikia
malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
“Utaratibu huu ulioboreshwa, ni
msisitizo na maelekezo ya Serikali ya mwezi Agosti 2011 kupitia
iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza Taasisi
zote za Elimu ya Juu nchini zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo
kuanzisha Madawati ya Mikopo ili kuongeza ufanisi katika utoaji
mikopo”,Alisema Ngole.
Ameongeza kuwa, dawati hilo
linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye sifa na
uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya Makamu Mkuu wa chuo
husika anayeshughulikia taaluma.
Meneja Ngole amesisitiza kuwa kwa
sasa vyuo vyote vina Maofisa Mikopo ambao wanawajibika kutafuta
suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.
Akifafanua hatua zinazotakiwa
kufuatwa na Maofisa hao katika kutafuta suluhisho la malalamiko ya
wanafunzi amesema kuwa, baada ya malalamiko kufika kwa Ofisa Mikopo
yanatakiwa yapate suluhisho ndani ya siku mbili tangu kuwasilishwa
kwake,ikiwa hatakua na ufumbuzi atatakiwa kuwasiliana na uongozi wa juu
wa chuo husika.
Endapo uongozi wa juu wa chuo
hautokuwa na ufumbuzi, malalamiko hayo yatatakiwa kupelekwa kwenye Ofisi
za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha na
Zanzibar au ofisi za makao ya makuu ya Bodi zilizoko jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment