Ndugu wakiwa kwenye kabuli la mpendwa wao Christian Benjamin Mlyansi.
Na Kalonga KasatiDAR ES SALAAM: Waafrika wanaosoma na kufanya kazi nchini India sasa wanaishi roho mkononi kutokana na matukio ya kudhalilishwa, kunyanyaswa na kuuawa kwa wenzao katika mazingira ya kutatanisha.
Hali ya hofu imezidi kuongezeka kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kudhalilishwa kwa binti Mtanzania (jina limehifadhiwa) anayesoma katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore nchini humo kwa kupigwa na kutembezwa mtupu mtaani.
Aidha, tukio la kijana Mtanzania, Christian Benjamin Mlyansi mwenyeji wa Tabora kukutwa Amefariki katika kile kilichodawa ni kupata ajali ya pikipiki nalo limewaacha na sintofahamu Waafrika waishio nchini humo.
Wakizungunza na Uwazi kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu juzi, baadhi ya Watanzania waishio India wameeleza hofu waliyonayo wakisema kuwa, matukio yanayoendelea kutokea yanawafanya Washindwe kuishi kwa amani.
“Hatuna amani kabisa, matukio ya hivi karibuni yametuacha kwenye wakati mgumu sisi Watanzania Na Waafrika kwa ujumla tunaoishi hapa.
“Vitendo vya Waafrika kudhalilishwa, kubaguliwa, kupigwa na kuuawa vimekuwa vikitokea na kuna Baadhi ya maafisa wa serikali ya India wamekuwa kama wanaunga mkono, jambo ambalo ni hatari Sana,” anaeleza Jamal Kasri mwenyeji wa Dar es Salaam anayefanya biashara katika Mji wa Bangalore.
Naye mwanafunzi Mtanzania anayesoma katika Chuo Kikuu cha Acharya, aliyeomba hifadhi ya jina lake ameliambia Uwazi kuwa, imefika wakati wanapokuwa mtaani au maeneo ya starehe wanakuwa Wanajificha kuogopa kwamba huenda wakafanyiziwa.
“Kiukweli hali si nzuri hapa India, usalama wetu ni wa mashaka.
Gari la mwanafunzi aliyedhalilisha India likiwaka moto.
“Hata kile kifo cha yule Christian Benjamini aliyekutwa amekufa, bado kina makengeza kwani wapo Wanaoamini kuna Mhindi aliyemsababishia ajali ile makusudi.”
Akizungumza na Uwazi kwa njia ya simu juzi, mmoja wa viongozi wa wanafunzi Watanzania Wanaosoma India, Bosco Thomsoni Mtani alisema baada ya matukio ya kifo na kudhalilishwa kwa Mwanafunzi, hali ilikuwa si ya amani na wengine walifikia hatua ya kutoenda chuoni.
“Tukio la kudhalilishwa kwa yule dada yetu na kifo cha Christian vimeacha hofu kubwa mioyoni Mwa wanafunzi na hata Waafrika waishio hapa India, tumewasiliana na Ubalozi wa Tanzania hapa ili kuona njia sahihi za kukabiliana na hali hii yenye rangi fulani ya ubaguzi,” alisema Bosco.
Mwaka 2010 lilitokea tukio la kusikitisha la kijana Mtanzania anayetokea Moshi aliyekuwa akisoma Nchini India, Imran Mtui ambaye alikutwa amechinjwa na kukatwa miguu na mikono katika eneo la Bangalore.
Mwaka 2013 pia kijana Mnigeria, Obodo Uzoma Simeoni, 36, aliuawa kikatili katika Kijiji cha Parra, Mji wa North Goa, India huku ubaguzi wa rangi ukitajwa kuwa chanzo.
Kufuatia sakata hilo, Balozi wa Tanzania nchini humo, John Kijazi alisema watahakikisha wanafunzi Wanaosoma India wanakuwa salama lakini akawataka nao kuheshimu sheria za nch
No comments:
Post a Comment