Wednesday, 10 February 2016

Benki ya Dunia kutengeneza miundo mbinu imara Temeke

msuNa Kalonga Kasati

Serikali kushirikiana na Benki ya Dunia inategemea kuanza ukarabati wa Miundo Mbinu mibovu Hususani  ya mitaro inayosababisha Maafa wilayani Temeke kuanzia mwezi Mei mwaka huu.
 Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wilaya ya Tem
eke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama  ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.

Hili limetokea baada ya uchunguzi uliofanyika jana ambapo Mhandisi wa Wilaya, Bwana Afya pamoja na Afisa Habari wa Wilaya walifika eneo la tukio na kuona hali halisi.
‘’Ni kweli maafa hayo yametokea na sababu hasa ni miundo mbinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika maeneo ya makazi ya watu,kwahiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi yanapostahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu’’Alisema Msumba.

Aliongeza kuwa ukarabati huo wa mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP) Unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Aidha, Joyce Msumba amesema kuwa endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza Watatumia njia ya kuyanyonya Maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea.

Mradi huu unalenga kuhamisha njia za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende moja kwa moja baharini.

Hilary Clinton “Apigwa”, Tajiri Donaldo Trump Ashinda Kura Za Mchujo


 
HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti
charais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo,
ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.
Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye
Mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne
usiku.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri Mkubwa kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa Wanaleta “shobo”

Nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich
aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted
Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.
Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari

Wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo. Clinton ambaye aliwahi
kuwa Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari
Amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye
kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic. 

Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

Kombe La Shirikisho Raundi Ya 16

Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16 bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.
Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.

Na Kalonga Kasati

Ijumaa tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi, Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex – Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Februari 28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Raundi hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Young Africans watawakaribisha JKT Mlale katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu Ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.

No comments:

Post a Comment