Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu
(kulia) na Jiji Mkuu Tanzania Mohammmed Chande Othman wakati
alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha
siku ya sheria Zanzibar.
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati
wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake
leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar
zilizofanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini
Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mohammed Othman Chande,
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW)
Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika sherehe za kilele cha
siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini
Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu
Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman
Chande, Baadhi
ya majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria
Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa
Wananchi katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Mwanasheria
Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha
jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati wa sherehe za kilele
cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya
Victoria Garden Mjini Unguja.
Kikundi
cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika
sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika
viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein ,{Picha na Ikulu.]
Siku 100 za Rais John Magufuli, Wagonjwa Muhimbili Wapata Dawa kwa Asilimia 96
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio
ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu
alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Waandishi wa habari na Madaktari wakifuatilia mkutano huo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Museru akisisitiza jambo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali hiyo.
Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa
MNH, Profesa Museru akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.
Na Kalonga Kasati
Wagonjwa anaotibiwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi sasa wanapata dawa kwa zaidi
ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa yaliopo hospitali hapa.
Mafanikio hayo yamekuja baada ya uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa.
“Wagonjwa wanaokosa dawa kwenye
maduka yetu, hospitali inanunua haraka ili mgonjwa apate dawa kwa
wakati. Kwa sasa ukosekanaji wa dawa hospitalini umepungua kwa kiasi
kikubwa sana kutokana na kuimarisha utendaji ndani ya hospitali,”
amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence
Museru.
Hayo yamesemwa leo na Profesa
Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya
hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu
alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Profesa Museru amesema kwamba
Katika muda wa kipindi cha miezi miwili Disemba 2015 na Januari 2016,
hospitali imefanikiwa kulipa wafanyakazi malimbikizo ya madai yao ambayo
walikuwa wakiidai hospitali hiyo kwa kipindi kirefu.
Malipo hayo ni malipo ya on call,
malipo ya wauguzi ya usiku, malipo ya posho mbalimbali hasa kwa
madaktari pamoja na kada nyingine za afya ambazo zinashughulika moja kwa
moja na wagonjwa.
Amesema kwamba kutolipwa kwa
malipo hayo kulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa na
kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kukosekana kwa tija
katika utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine, Profesa
Museru amesema kwamba mapato kwenye hospitali hiyo yameongezeka kwa
zaidi ya asilimia 60 baada ya Disemba hospitali hiyo kuzalisha Shilingi
bilioni 3.3 kutoka wastani wa shilingi 2.7 zilizokusanywa miezi mitano
(Julai 2015 hadi Novemba 2015)
“Mwezi Disemba mwaka jana
tulizalisha shilingi bilioni 3.3 na Januari 2016 tulizalisha shilingi
bilioni 4.3,” amesema mkurugenzi huyo.
Akizungumzia mashine za CT-Scan
na MRI, Profesa Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Magufuli ilinunulia Hospitali hiyo mashine mpya ya
CT-Scan yenye uwezo wa 126 slices.
“Uwapo wa mashine hii mpya
umeongeza uwezo kwa kiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwa wakati
mmoja. Sasa tunaweza kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde
sita. Awali tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakini sasa
tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa 24.
“Baada ya kuwapo kwa mashine hizi
mbili za CT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwa vipimo
vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hii mpya ambayo ni ya kisasa
zaidi na yenye nguvu kubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamu
zaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kama moyo, utumbo, ubongo na
hivyo kupata majibu sahihi ya chunguzi na uhakika zaidi. Mashine hii
mpya tangu ilipofungwa Novemba 26, 2015 hadi Februari 9, 2016 imepima
wagonjwa 863,” amesema Profesa Museru.
Amesema kwamba baada ya mashine
ya MRI kutengenezwa wagonjwa zaidi ya 2,200 wamepimwa na kwamba baada ya
mashine ya CT-SCAN kutengenezwa wagonjwa zaidi 1,000 wamepatiwa vipimo.
No comments:
Post a Comment