Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam
kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi
wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Nibu Waziri Fedha na Mipango Dkt.
Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini
jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi
katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika
kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum
Shamte (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha
na Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali
inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili
kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Katikati ni
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,
Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara
nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta
binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi
katika kupata huduma za jamii.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa
katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu
Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi
ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa
katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu
Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi
ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali imesema dhamira yake ya
kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia maeneo ya vipaumbele
ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha
2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya
misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia wananchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha
na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na wafanyabiashara
nchini jijini Dar es salaam.
Dkt. Mpango aliyaeleza maeneo
hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo ni
pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao
wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.
Maeneo mengine ni miradi mikubwa
ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili kuweza kupata matokeo
makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo maeneo maalum ya
kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na Mtwara kutokana na maliasili
iliyopo hapo.
Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango
aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia malighafi
inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa ni
msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.
Katika suala la ujenzi wa reli ya
kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema kuwa mradi huo ni
muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji ndani na nje ya
nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) na mataifa mengine.
Mafanikio ya ujenzi wa viwanda
nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria kushirikiana na
serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana na
maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya
viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.
Aidha, ili kujenga uwezo wa kuwa
na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi ambayo ndiyo
msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha ambapo
wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya
usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika mkutana huo, Dkt. Mpango
amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara yao ili kuwa na
kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza wafanyabiashara
wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia wanapouza bidhaa
zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine hizo,
Serikali inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.
Vile vile, Dkt. Mpango ametoa
namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Mambo ya
Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi nzima kwa
namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.
Aidha, Dkt. Mpango amewaonya
wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache kufanyabiashara za magendo
ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa
bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati na Sera TPSF Felix Mosha amesema kuwa Sekta binafsi itaendelea
kushirikiana na Serikali katika mpango wa kukuza uchumi wa nchi na
kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa watatimiza wajibu wao wa
kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini wanakwenda pamoja
na Sera ya “Hapa Kazi Tu”.
No comments:
Post a Comment