Tuesday 29 August 2017

Trump aja kivingine tena

Rais wa Marekani Donald Trump ameondoa marufuku iliowekwa na Obama kuhusu kuwapatia maafisa wa polisi vifaa vya kijeshi.
Agizo hilo la rais sasa litawaruhusu maafisa wa polisi kupokea vifaa vya kijeshi ikiwemo magari ya kijeshi na kofia zisozoweza kuingia risasi.
Mwanasheria mkuu Jeff Sessions amesema kuwa lengo lake kuu ilikuwa kuimarisha usalama miongoni mwa raia.
Bwana Obama alilizuia jeshi kutowapatia maafisa wa polisi vifaa vyake kufuatia mgogoro wa Missouri.
Marufuku hiyo ilifuatia shutuma kwamba maafisa wa polisi walikuwa wazito kupitia kiasi kukabiliana na waandamanaji kufuatia mauaji kijana mmoja mweusi yaliotekelezwa na polisi mzungu 2014.
Rais huyo wa zamani alikuwa na wasiwasi kuhusu maoni ya raia kuhusu maafisa wa polisi waliovalia magwanda mazito ya kijeshi akisema kuwa ilikuwa muhimu kwamba maafisa wa polisi walifaa kuonekana kuwa miongoni mwa jamii badala ya kuonekana kuwa maadui.

Lakini bwana Sessions alidai kwamba hatua hiyo ya Obama ilikuwa imepita mipaka.

No comments:

Post a Comment