Sunday 27 August 2017

Mkapa: Bara la Afrika linatakiwa kujiamini.

Rais Mstaafu Mh.Benjamin Mkapa amesema Bara la Afrika linatakiwa kujiamini,kuonesha utashi mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kuwa nchi za Afrika zinaweza kutafutwa na kusikilizwa katika masuala mbalimbali yanayohusu amani na usalama.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amesema hayo wakati akifunga mkutano wa 4 wa uongozi wa Afrika kuhusu masuala ya amani na usalama nchini Afrika Kusini,ambapo pia ametoa changamoto kwa vyombo vya habari kuonesha uzalendo kwa kuandika habari zinzolinda masalahi ya taifa.
Mapema Mwenyeji wa Mkutano huo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki alisema kazi kubwa iliyopo ni kuipa uweza umoja wa Afrika wa kukabiliana na changamoto za uvunjifu wa amani na usalama katika nchi mbalimbali za Afrika badala ya kuiachia umoja wa mataifa kwani matatizo ya Afrika yanapaswa kutatuliwa na waafrika wenyewe.

Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na Marais wastaafu saba akiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, Olusegun wa Nigeria, Bakili Muluzi wa Malawi,Muhammed Mojcef Marzouki wa Tunisia na Hassan Sheikh Mohammed wa Somalia.

No comments:

Post a Comment