Saturday 22 July 2017

IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia sheria

1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
IGP Sirro, ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na askari na maofisa wa mkoa wa Kagera, wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.
Alisema kuwa, kila askari analojukumu mbele yake la kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.
Hata hivyo, katika ziara yake, IGP Sirro, amewahakikishia askari na maofisa kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.
 
Aidha, katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

No comments:

Post a Comment