Monday 24 July 2017

Ronaldo amwambia Neymar "usiende PSG timu ndogo"

Cristiano Ronaldo amemwambia Neymar asijiunge na Paris Saint-Germain kama anataka kuondoka Barcelona aisubili kwanza Manchester United.
Ronaldo amemwambia nyota huyo wa Barcelona atakuwa amefanya kosa kubwa kama ataamua kuhamia Ufaransa kwa sasa.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amedai ni bora Mbrazili huyo akachukua uamuzi wa kuhamia Manchester United kama kweli amedhamilia kuondoka Nou Camp.
Ronaldo na Neymar ni marafiki wa karibu mbali ya ushindani wa timu zao, urafiki huo unatokana na wawili hao kuwa chini ya udhamini moja wa Nike.
Jarida la Hispania la Diariogol limedai kuwa nyota hao wawili wamekuwa na mazungumzo ya karibu kuhusu uhamisho huo wa pauni 195milioni wanazotaka kutoa PSG.
Wamedai kuwa Ronaldo alimtumia ujumbe mzito kwa WhatsApp akimtazalisha nyota huyo mwenye miaka 25, kutofanya uamuzi wa kuhama kutoka La Liga kwenda Ligue 1.
PSG wamehaidi kumlipa mshambuliaji huyo pauni 500,000, kwa wiki na klabu hiyo ya Paris ikipanga kumtumia yeye kujitangaza duniani.
Lakini wamedai kuwa Ronaldo amemwambia Neymar atakuwa amerudi nyuma kuhamia katika klabu ndogo.
Mwanasoka huyo bora wa dunia anaamini ni Real na Manchester United ndizo zenye hadhi sawa na Barca duniani.

Neymar kwa sasa yuko Marekani na Barcelona katika maandalizi ya mwanzo wa msimu, alifunga mabao mawili wakati miamba hiyo ya Hispania ikichapa Juventus 2-1 jijini New York.

No comments:

Post a Comment