Monday 24 July 2017

IGP Simon Sirro, amewataka askari kuhakikisha wanatenda haki wakati wakitekeleza majukumu yao

1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, wakati alipomtembelea ofisini kwake jana, IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi, yenye lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza,  John Mongella, wakati alipofika ofisini kwake jana, IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi, yenye lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo, kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi.
3 (2)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, kwa lengo la kujitambulisha, IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, alipofika kwa lengo la kujitambulisha, IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
6
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo mara baada ya kumaliza kikao kazi na maofisa na askari ambapo aliwasisitiza kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo kuhakikisha wanatenda haki wakati wakitekeleza majukumu yao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha, IGP Sirro, ametoa wito kwa wananchi na raia wema kuendelea kutoka ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti matishio mbalimbali ya uhalifu yanayoweza kujitokeza katika maeneo yao.


IGP Sirro, ameyasema hayo akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza, ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na askari wa Jeshi hilo ikiwa pamoja na kujitambulisha kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.

No comments:

Post a Comment