Friday 21 July 2017

Lissu kutopelekwa Mahakamani

Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume 
  Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema mpaka sasa hajaruhusiwa kumuona mteja wake licha ya kufika Polisi Makao Makuu tangu asubuhi.
Akizungumza leo Ijumaa, Julai 21, Karume aliyekuwa na wakili mwingine wa Chadema, Peter Kibatala amesema wameambiwa Lissu hatapelekwa mahakamani kwa sasa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
“Tupo hapa tangu asubuhi, tunaambiwa hatuwezi kumuona kwa sasa, lakini jambo la kushangaza ni kuwa tunaambiwa hatapelekwa mahakamani kwa kuwa uchunguzi haujakamilika ingawa kosa bado halieleweki,” amesema.
Amesema polisi wamewaambia mawakili wa Lissu kuwa hata dhamana kwa leo haitawezekana kwa sababu upelelezi haujakamilika.

No comments:

Post a Comment