Wednesday 26 July 2017

Marekani Kama Mbwayi mbwai kwa Urusi, Iran na Korea Kaskazini


Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora.
Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anashutumiwa kwa kuibua silaha hatarishi za nyuklia kila kukicha.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anashutumiwa kwa kuibua silaha hatarishi za nyuklia kila kukicha.
Akizungumza katika baraza hilo wawakilishi David Ciciline kutoka chama Democratic amesema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.
Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.
Naye Ted Poe kutoka chama cha Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia.

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameahidi kuondoa migogoro ya kimataifa inayoikabili nchi hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la Urusi Duma , Leonid Slutsky amesema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani.

No comments:

Post a Comment